Skip to main content

Posts

Showing posts from May 11, 2017

HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KATIKA KUZIPA HADHI HOTELI

Hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini hoteli fulani inatajwa kuwa ni ya nyota tatu, nne au tano? Najua itakuwa ni vigumu kuelewa kama haupo katika tasnia ya masuala ya hoteli au utalii mpaka upatiwe ufafanuzi wa kutosha. Hivi karibuni Serena Hotel ya jijini Dar es Salaam ilifanikiwa kupewa hadhi ya kuwa hoteli ya nyota tano katika hafla ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe. Umuhimu wa kuzipatia hadhi hoteli husaidia sana kuchochea ushindani katika biashara hasa kwa upande wa uboreshaji wa huduma.  Kupitia makala haya Jumia Travel imekukusanyia vigezo ambavyo mara nyingi huzingatiwa mpaka hoteli kupewa hadhi fulani.  Nyota moja. Mara nyingi hoteli hizi humilikiwa na watu binafsi katika utoaji wa huduma za malazi kwa wateja. Huwa ni ndogo na za ukubwa wa saizi ya kati zikipatikana katika maeneo ambayo gharama za maisha ni ya kawaida kabisa.  Kikubwa kinachozingatiwa ni kuweza kukidhi...

WOTESAWA KUFANYIKA SENSA YA WAFANYAKAZI WA NYUMBANI

Jackline Ngalo ambaye ni Mwanasheria wa shirika la kutetea Haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini, WOTESAWA, akizungumza na Lake Fm, baada ya semina kwa viongozi wa serikali za Kata/Mitaa pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza ili kuwajengea uwezo wa kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani katika maeneo yao. Na Binagi Media Group Semina kwa viongozi wa serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza ikiendelea Jijini Mwanza Semina hiyo imeandaliwa na shirika la WOTESAWA kwa siku tatu tangu Mei 09 hadi leo Mei 11,2017 Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza mwanahabari Nashon Kenedy, wakati akichangia mada kwenye semina hiyo Wadau wa Maendeleo mkoani Mwanza wameidhinisha mikakati mbalimbali ikiwemo kufanya sensa ya watoto wafanyakazi wa nyumbani na utungwaji wa sheria ndogo ndogo za kuwalinda watoto, lengo likiwa ni kusaidi...

MAGAZETI LEO IJUMAA

Good Morning mtu wa nguvu, leo ni May 12 2017. MAGAZETI KWA HISANI YA QUEEN ESTER  TOWER HOTEL YA IRINGA