Skip to main content

Posts

Showing posts from December 22, 2016

MBUNGE VITI MAALUM RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo Mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo. Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana  Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili. Na fredy mgunda,Iringa Mb...

MEYA DAR ES SALAAM AWAONYA WAKUSANYA USHURU WA MAEGESHO

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akifafanua jambo kwa wandishi wa habari leo kuhusiana na suala zima la tozo za maegesho ya magari MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewataka wakandarasi hususani wanaokusanya ushuru wa maegesho, waanze kutumia mashine za EFDs walizokabidhiwa vinginevyo mikataba yao iko hatarini kusitishwa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Meya Mwita amesema kwa muda mrefu wakandarasi hao walikuwa wakitumia mashine za mkono, wamebaini mapato mengi yalikuwa yakipotelea mifukoni mwa watu wachache na sasa ni agizo kwa wazabuni wote wa wilaya za Daresalaam kutumia mashine za Kielectroni. Amesema kupitia mashine hizo wanahakika mapato yataongezeka kutoka shilingi milioni 170 iliyokuwa inakusanywa hapo awali kwa mwezi hadi kufikia Zaidi ya Shilingi Milioni 370 kwa mwezi. Katika hatua Nyingine, Isaya Mwita amewaonya wakandarasi hao kuangalia namna ya kuwadhibiti wafanyakazi wao kwani hivi sasa wamezusha tabia ya kuwany...

MAZISHI YA KIHISTORI IRINGA MAREHEMU AZIKWA KABURI MOJA NA KONDOO

Wanafamilia wakiwa wamelizungika kaburi la marehemu Ngaga aliyezikwa kaburi moja na kondoo pamoja na kuku mweusi leo kwenye kitongoji cha Mkawaganga kijiji cha Mbigili wilaya ya Kilolo mkoani Iringa  Mganga wa kienyeji Galasiano Nyenza (kulia) akiwa na mtoto wa marehemu Andrea Ngaga ,Kurugenzi Ngaga kushoto baada ya kufanyika kwa mazishi ya kimila katika kijiji cha Mbigili Kilolo kwa marehemu kuzikwa kaburi moja na kondoo na kuku mweusi  Mganga Nyenza aliyeongoza mazishi hayo katikati akiwa na baadhi ya ndugu kando ya kaburi  Waombolezaji wakitoka kuzika     Marehemu enzi za uhai wake  Nyumbani kwa marehemu waombolezaji wakiwa kwenye foleni  .................................................................................................... Na MatukiodaimaBlog MAMIA ya wakazi wa kijiji cha Mbigili na mji wa Ilula katika wilaya ya Kilolo wamefurika katika mazishi...

KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA LA MKOA WA IRINGA KINAENDELELEA...

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu akisoma taarifa kutoka sekta binafsi wakati wa kikao cha baraza la biashara cha mkoa wa Iringa kinachofanyika mjini Iringa leo. (Picha na Friday Simbaya) Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha baraza la biashara cha mkoa wa Iringa wakifuatilia kikao hico kwa makini kinachofanyika mjini Iringa leo. (Picha na Friday Simbaya) Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Mkoa wa Iringa akifungua kikao cha baraza hilo kinachofanyika mjini Iringa leo. Walioketi kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa Lucas Mwakabungu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa (RAS) Wamoja Ayubu (Picha na Friday Simbaya) Mweka Hazina kutoka TCCIA Iringa ambaye pia ni mmoja ya wajumbe wa sekretatrieti akisoma taarifa wakati wa Kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Iringa (RBC). Sekretarieti, kushoto niJames sizya mtendaji TCCIA (M) Iringa na Rose mjumbe. Baadhi ya wa...