Skip to main content

Posts

Showing posts from February 28, 2016

SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS

Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning Nathow. Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam. Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara. Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha a...

MAGAZETINI LEO JUMATATU

MBEYA CITY FC WAAGA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO

TIMU ya Mbeya City FC Jumamosi hii imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup 2015/16) inaendelea katika mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora. Jumamosi Februari 27, kulikwa na michezo nane iliyochezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo, Mwadui FC ilicheza na maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons ilicheza na Mbeya City na kubamizwa bao 2-1 katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine jijini hapa.  Kwa mantiki hiyo Mbeya City FC imetolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa an Tanzania Prisons bao 2-1, na kufanya Tanzania Prison kusonga mbele katika hatua nyingi ya michuano hiyo katika uwanja sokoine uliyojaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha. Kutokana na hali hiyo wachezaji walicheza chini ya viwango kutokana na uwanja huo kuteleza na kufanya wachezaji wa timu zote mbili kushindwa kuonyesha kandanda safi. Katika mchezo huo, Tanzania Prisons ilianza kupat...