Mbunge Mteule wa Viti Maalum Vijana Taifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka mkoa wa Iringa, Jasmine Ng’umbi, ameahidi kutumia nafasi yake bungeni kuhamasisha na kusukuma mbele miradi inayowagusa moja kwa moja vijana na wanawake, ili kuongeza fursa za maendeleo kwa makundi hayo. Akizungumza leo wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akizindua kampeni za wagombea ubunge na udiwani katika majimbo ya Kalenga na Iringa Mjini, Jasmine alisema anaingia bungeni akiwa na dhamira thabiti ya kuhakikisha vijana na wanawake wanapata nafasi kubwa zaidi kiuchumi na kijamii. “Nitashirikiana na Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan na wabunge wenzangu kuhakikisha tunatunga na kusimamia sera zenye kutoa matokeo chanya kwa vijana na wanawake, kuanzia upatikanaji wa mitaji midogo, ujuzi wa kisasa, hadi ushiriki kwenye miradi mikubwa ya maendeleo,” alisema. Jasmine aliwataka wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanampa kura za kishindo Dkt. Samia, wabung...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.