Skip to main content

Posts

Showing posts from October 18, 2015

Guinea Divided as Conde Re-Elected

People sit inside a local restaurant displaying posters for Guinea’s incumbent President Alpha Conde, in Conakry, Guinea, Oct. 17, 2015. Guinea's incumbent President Alpha Conde won the country’s second democratic election, but Guinea’s opposition parties have rejected the results and called for demonstrations. Bakary Fofana Fofana, the head of Guinea’s Independent National Electoral Commission, announced President Alpha Conde’s re-election victory late Saturday. Fofana said before the constitutional court’s final validation of the results, the electoral commission proclaims Conde as the winner in the first round of voting held last Sunday. Before the results were announced, Guinea’s main opposition leader and former Prime Minister Cellou Dalein Diallo announced he and the six other opposition candidates would reject them. FILE - Guinea's leading presidential candidate Cellou Dalein Diallo at the People's Hall in Conakry, Guinea, Sept. 21, 2010. ...

AMKA NA SIMBAYABLOG, MAGAZETI LEO JUMATATU

TUNAANGALIA MAJINA YETU...!

Wakazi wa mtaa wa Isoka B ambao hata hivyo hawakuhamika majina yao katika Kata ya Mwangata, Jimbo la Iringa mjini wakiangalia majina yao katika orodha ya majina ya wapiga kura katika kituo hicho cha kupigia kura jioni hii.

Mwalimu ampiga mwandishi

  Mwalimu Willibroad Samson wa Shule ya Sekondari Kitunda iliyopo Wilaya ya Ilala, akimdhibiti mwanafunzi, Elia Simion aliyekuwa akipigana na mwenzake. Picha na Tumaini Msowoya  Kwa ufupi Msowoya alipigwa na mwalimu aliyefahamika kwa jina la Willibroad Samson alipokwenda shuleni hapo kufuatilia madai kwamba baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, wiki iliyopita waliandikishwa na kupewa vitambulisho vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao. By Mwandishi wetu, Mwananchi Dar es Salaam.  Mwandishi wa Mwananchi, Tumaini Msowoya jana alipigwa ngumi kadhaa kichwani na mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitunda wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi. Msowoya alipigwa na mwalimu aliyefahamika kwa jina la Willibroad Samson alipokwenda shuleni hapo kufuatilia madai kwamba baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, wiki iliyopita waliandikishwa na kupewa vitambulisho vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Msowoya alisema kwa...

Masenza: Orodha ya vituo imepungua toka 1,641 hadi 1,601

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema orodha ya vituo imepungua kutoka 1,641 hadi kufikia 1,601, sawa sawa na vituo 40 vilivyopungua, Nipashe imedhibitisha. Alisema kuwa awali Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitoa orodha ya vituo 1,641 vitakavyotumika katika zoezi la upigaji kura kwa Mkoa wa Iringa kwa Halmashauri zote tano (5).  Masenza alisema hayo wiki iliyopita wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.  Alisema kuwa idadi hiyo imepungua kufikia vituo 1,601 baada ya uhakiki wa wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaoendelea kufanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi. Alisema kuwa halmashauri zote zimepokea vifaa kama masanduku, mifuniko, Tshirts, kofia, Vituturi, na fomu mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.  Aidha, alisema kuwa wasimamizi wanaendelea kufanya tathmini ili kujiridhisha endapo vifaa vilivyopokelewa vinakidhi mahitaji. “Tayari ...

KUJISAIDIA PORINI KWA WASAFIRI SASA BASI...!

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akikagua ujenzi wa mradi. Dkt Mohamed Gharib Bilali (Picha n a Friday Simbaya) Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali amesema tabia ya kujisaidia porini kwa wasafiri kama wanyama kwa lugha maarufu ya “kuchimba dawa,” sasa basi, baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini. Alisema kuwa kwa muda mrefu abiria wanaosafiri katika barabara kuu, wamekuwa wakipata taabu pindi wanapohitaji sehemu za faragha. Dkt Bilali alisema hayo katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. Mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini unakusudia kujenga vituo vya mapumziko kwa wasafiri 44 nchi nzima katika barabara kuu zote nchini. “Jambo hili limefikia katika hatua mbaya hata kukiuka ustaarabu...

DKT BILALI AWEKA JIWA LA MSINGI MRADI WA VITUO VYA MAPUMZIKO KWA WASAFIRI NCHINI

Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana.  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Generali Raphael Muhuga  kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Davis  Mwamuyange  akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi mbela ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara kuu nchini katika hafla fupi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero wilayani Mufindi, mkoani Iringa jana. Mradi huo unatekelezwa na Mufindi Environmental Trust (MUET) kwa kushirikiana JKT. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA ) Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali  akiwaaga wananchi wa Kijiji cha Idetero baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa vituo vya mapumziko na vyoo kwa wasafiri katika barabara k...