Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza. Na:George Binagi-GB Pazzo +BINAGI MEDIA GROUP Chama cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Nchini OJADACT, Kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi yake ya kufanyia marekebisho sheria kandamizi kwa vyombo vya habari nchini, aliyoitoa wakati wa Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana. Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko, ametoa ombi hilo hii leo mbele ya Wanahabari Jijini Mwanza, wakati akielezea hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali dhidi ya vyombo vya habari vinavyokiuka sheria katika utendaji wake wa kazi. Soko alitolea mfano Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kupitia sura ya 229 kifungu cha 25 (1), kinachompa Mamlaka Waziri wa Habari kulifungia gazeti lolote linalotoa habari zenye ukakasi, kuwa ni ishara ya ukandamizaji wa uhuru wa habari ...