Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde. Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), limetangaza matokeo ya kidato cha pili huku msichana, Lineth Christopher kutoka Shule ya Sekondari ya St. Aloysius Girl’s ya mkoani Pwani, aking’ara kitaifa. Matokeo hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Charles Msonde, ambaye alisema waliofanya mtihani huo mwaka jana walikuwa ni wanafunzi 363,666 sawa na asilimia 91.66. Alisema kati ya walioufanya mtihani huo, waliofaulu ni wanafunzi 324,068 sawa na asilimia 89.12, ambapo wasichana ni 164,547 sawa na asilimia 89.00 na wavulana ni 159.521 sawa na asilimia 89.24. Dk. Msonde alisema wanafunzi 39,567 sawa na asilimia 10.88 walishindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya Kidato cha tatu; hivyo watarudia darasa wakati wanafunzi 33,104 sawa na asilimia 8.34 hawakufanya mtihani huo kwa sababu za utoro na magonjwa. Alisema idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa mad...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.