Skip to main content

Posts

Showing posts from September 15, 2016

KAMPUNI YA KUJENGA BARABARA YA DEL-MONTE YAENDELEA KUKATALIWA JIJINI DAR

Pichani ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Ngumilamoto akifafanua jambo na waandishi wa habari (Picha na Maktaba) NAIBU meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Ngumilamoto amesema wataiondoa kwenye tenda Kampuni ya ujenzi wa Barabara Del-Monte katika manispaa hiyo baada ya kujiridhisha kampuni hiyo inafanya kazi chini ya kiwango ikiwemo kuchelewesha kumaliza kazi kwa wakati.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo, Kauli ya Ngumilamoto inakuja ikiwa ni tayari mkuu wa mkoa wa Dare s Salaam,Paul Makonda ambaye naye aliiagiza viongozi wote wa manispaa ya mkoa huo kutoipa tenda kampuni ya Del-Monte kutokana na kujenga barabara nyingi chini ya kiwango. Ngumilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti kupitia chama cha Wananchi (CUF) ameyasema hayo leo wakati alipokuwa anafanya ziara na Kamati ya fedha ya Manispaa hiyo kwenye miradi mbali mbali iliyoanza kutekelezwa ili kujilidhisha juu ya ufanisi wake.  Amesema Kampuni hiyo ilipewa tenda ya kujeng...

TETEMEKO LA ARDHI: MAJALIWA AWAANGUKIA WAFANYABIASHARA NA MABALOZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016.  Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera. Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:- Ubalozi wa China – Milioni 100 Ubalozi wa Kuwait – Euro 10,000 Ubalozi wa Kenya- wametoa mabati na malazi Kampuni ya China Mercharnt Group – Mil 100 Mo Dewji – Milioni 100 Toyota Ltd – Milioni 10 TBL – Milioni 100 Woolworth -Milioni 20 Sahara Tanzania – Milioni 20 Azania Group – Milioni 20 Kagera Sugar -Milioni 100 na Tani 10 za sukari Nosime Group- Milioni 75 Tanga Cement – Mifuko 1000 ya Saruji Reginald Mengi – Milioni 110 Protas Ishengoma- Wakili na mhanga wa tetemeko Milioni 5 GBP, MOIL,&OILCOM- Watajenga shule mbili zilizoharibika Vile ...