Skip to main content

Posts

Showing posts from October 6, 2010

JAMANI, JAMANI AJALI HIZI ZITATUMALIZA

Basi la kampuni ya Hood lenye nambari za usajili T249 ARU likiwa limepinduka katika barabara kuu ya Iringa -Mbeya (Tanzam) eneo la Viwengi Wilaya ya Kilolo  mkoani Iringa,  basi hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya na katika ajali hiyo watu zaidi ya 20 wamejeruhiwa japo hakuna hata mmoja aliyepoteza maisha katika ajali hiyo. Thanks God it has not killed anyone but  sorry for injured persons, still we need to control this kind of accidents in future by put up stiff punishment to drivers who wreckless and overspeeding.

LIVE IN SONGEA

  Ikiwa ni jua kali mchana leo, wakina mama wakiwa wamepanga biashara  yao ya dagaa wakutoka Ziwa Nyasa ndani ya stendi kuu ya mabasi katika Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma wakisubiria wateja wakinunua , ambapo kilo moja ya dagaa hao walikuwa wanauuza kwa  shilingi elfu moja na mia tano (1,500/-). Mabasi na magari yanayotumia kituo hicho hupita kwa shida sana kutokana na wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wanaouuza chai na vya chakula kupanga biashara zao sehemu ya kupitia magari kama inavyoonekana katika picha.   Sehemu ya 'shamba la wafu' walipozikwa masista na mapadre wakizungu kwa miaka ya nyuma sana katika makaburi yaliyopo karibu na Kanisa Kuu la Katoliki ya PeramihoWilayani Songea yakionekana kuzungushiwa 'wire fence' ni moja ya vivutio vya utalii katika Mkoa Ruvuma. Makaburi haya yana historia ndefu ya umisionari wa katoliki pamoja na mambo ya kadha wa kadha. Hebu jaribu kuyatembelea siku moja utashangaa mwenyewe....