Skip to main content

Posts

Showing posts from June 26, 2017

ASKOFU WA KKKT DK SHOO ASIFU UTENDAJI WA MAGUFULI

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amesema Mungu amemjalia Rais Dkt John Pombe Magufuli roho ya kutokuwa na hofu katika utendaji kazi zake. Askofu Shoo alisema hayo wakati akimwekwa wakfu na kuingizwa kazini Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa jana mjini Iringa.  Alisema kuwa Watanzania walio na nia njema, wanakuelewa na kukubali, na kanisa tunakuombea na tutaendelea kukuombea uzidi kuwa na ujasiri huo, ili Mungu akupe afya njema na usiache kusimama katika lile la kweli kama mwenyewe unavyosema msema kweli ni mpenzi wa Mungu.  Askofu alimalizia kwa kusema, ‘’Tunamuomba Mungu azidi kukupa washauri wema, washauri wasio na unafiki, wasio na hila na malengo ya kujinufaisha binafsi, washauri ambao wanajikomba komba lakini wakiwa na ajenda binafsi.  Ibada ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iring...

ASKOFU MTEULE GAVILLE AMTAKA RAIS MAGUFULI KUUMALIZIA MCHAKATO WA KUANDIKWA KWA KATIBA MPYA

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amemweka wakfu na kumwingiza kazini Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville jana huku akimtaka Rais Dk John Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya. (Picha na Friday Simbaya)