Skip to main content

Posts

Showing posts from November 25, 2010

Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete atangaza Baraza La Mawaziri

JK ATEUWA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete Katika Muundo wa Serikali hakuna mabadiliko makubwa isipokuwa yafuatayo: 1. Idara ya Umwagiliaji tumeiunganisha na Kilimo ambako ndipo ilipokuwa zamani. 1. Imeonekana upangaji wa maendeleo ya kilimo unakuwa hauna hakika bila ya umwagiliaji kuwa sehemu ya kilimo. Tuliihamishia maji kurahisisha pia upangaji na hasa kwa vile maji ndiyo wanaotoa haki ya matumizi ya maji. 2. Kwa kuwa tatizo la uhaba wa maji ya binadamu ni kubwa sana na tunataka tuongeze kasi ya kukabiliana na tatizo hilo tumeona tuiondolee wizara hii mzigo wa umwagiliaji ili ibaki na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa watu wanapata maji safi na salama mita 400 kutoka wanapoishi. 2. Idara ya Vijana tumeihamisha kutoka Wizara ya Kazi na kuihamishia Wizara ya Habari kwa sababu kuu 2. 1. Kwanza inashabihiana na michezo na utamaduni. 2. Tunataka Wizara ya Kazi ipate muda wa kutosha wa kushughulikia masuala ya ajira na wafanyakazi ambayo sasa yamepanuka. 3....

WAKONSOLATA NA HARAKATI ZA KULETA MAENDELEO HAPA NCHINI

UJIO WA WAMISIONARI WA SHIRIKA LA WAKONSOLATA NA HARAKATI ZA KULETA MAENDELEO HAPA NCHINI; Ujio wa wamisionari wa shirika la Wakonsolata hapa nchini mwishoni mwa karne ya 18, umetoa changamoto kubwa katika nyanja za maendeleo pamoja na kuleta chachu muhimu kwa jamii ya wananchi wa hapa nchini kutokana na wamisionari hao kujikita zaidi katika shughuli za kijamii na kuifanya jamii ya wananchi katika maeno ambayo walifika ambapo mkoa wa Iringa ni mmoja ya sehemu ambazo mabadiliko ya kimaendeleo hayo yamesababishwa na ujio huo. Wamisionari hao wa shirika la wakonsolata waliofika hapa nchini hususani mkoani Iringa, walikuwa ni mapadre, mabruda, masista na walei ambao kwa mara ya kwanza walifika kijiji cha Tosamaganga ambapo walifanya masikani yao na pia wote kwa pamoja walikuwa na lengo la kumkomboa binadamu wa kiafrika wa Tanzania na pamoja na shughuli zingine zote walizofanya za kijamii kiuchumi, kielimu, afya, mawasiliano walizingatia roho yao ya sala na kazi. Ingawaje shughuli zao...