MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas , amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, huku akiwatoa hofu juu ya uvumi unaoenezwa mitandaoni kuhusu uwepo wa vurugu siku ya uchaguzi huo. Asas amesema kumekuwepo na taarifa zisizo sahihi kutoka kwa baadhi ya watu, ndani na nje ya nchi, wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano na kuchochea vurugu ambazo zinaweza kuhatarisha amani na kuathiri zoezi la uchaguzi. Akihutubia maelfu ya wanachama na wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM Jimbo la Mafinga Mjini, uliofanyika katika kijiji cha Ugute, kata ya Isalavanu, Halmashauri ya Mji Mafinga, Asas aliwahakikishia wananchi kuwa nchi ipo salama na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kulinda amani. “Nataraji katika siku hizi mbili mtajitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 29. Msiogope wala kuwa na hofu, amani ipo na kutakuwa na ulinzi wa kutosha. Nchi yetu imetulia — hayo yote ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.