KIKWETE AKATA MZIZI WA FITINA KUHUSU GARI LA WAGONJWA MLANGALI AWALI WANANCHI WALIJIPANGA BARABARANI KUKUMBUSHA AHADI YA RAIS, MADIWANI WAPIGWA MSHANGAO
Ludewa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete jana alikata mzizi wa fitina kutokana na utata uliokuwepo kati ya wananchi na Baraza la Madiwani kuhusu gari la wagonjwa Namba SM 9192 aliloahidi kwa Kituo cha Afya Mlangali mwaka 2008. Dr. Kikwete alifikia hatua hiyo baada ya wananchi wa Kata ya Mlangali waliokuwa wamesimama barabarani kumlaki na alipowataka watoe shida zao wakamwambia kuwa wanashukuru kwa kutimiza ahadi ingawa wameipata jana wakati gari hilo lina zaidi ya miezi saba wilayani. Wananchi wa Mlangali pamoja na mambo mengine walimwambia Rais kuwa katika Kata yao wanakabiliwa na mambo mengi ikiwemo maji safi, barabara, gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) na umeme. Madiwani katika kikao chao cha Julai 15 mwaka huu walikubaliana kwa kauli moja kuchukua gari la kubebea wagonjwa (Ambullance) No. SM 4677 lililokuwa katika Hospitali ya Wilaya na kulipeleka Lupingu ili kuwahudumia wananchi wa Mwambao na gari SM 9192 lililotolewa ...