Skip to main content

Posts

Showing posts from March 10, 2016

RADIO MPYA YA WANANZENGO JIJINI MWANZA, KUANZA KURUKA HEWANI RASMI

Imethibitika kuwa Hit Radio Station ijulikanayo kwa jina la LAKE FM ya Jijini Mwanza inatarajia kuanza kuruka hewani rasmi kupitia 102.5 kuanzia wiki ijayo. Redio mpya ya wananzengo Mkoa wa Mwanza itakua hewani rasmi kuanzia jumatatu wiki ijayo Machi 14, 2016.  Tunaposema Raha ya rock city unaelewa nini? Follow @lakefm_mwanza kucomment ili tujue mapokeo yako.  #LakeFM #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo.

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA AFYA BURE KUTOKA KWA BANGO SANGHO

Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam. Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) unataraji kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, upimaji utakaofanyika Jumapili ya Machi, 13 katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam. Akizungumzia huduma hiyo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee amesema huduma hiyo itawawezesha wazazi kutambua magonjwa yanayowakabili watoto wao bila kulipa malipo yoyote kwa kutambua umuhimu wa afya ya watoto kwa maendeleo ya taifa...