Skip to main content

Posts

Showing posts from June 20, 2016

Watanzania wapata fursa ya kushiriki mafunzo kuhusu Tsunami

Kutokana na kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga. Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine. "Watu wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa," alisema Bi. Rodrigues. Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata ...

Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero. Tanzania yatajwa katika nchi zinazoongoza kwa unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino. Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji. Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino. "Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata k...