Skip to main content

Posts

Showing posts from August 6, 2016

MSHINDI WA AIRTEL TRACE MUSIC STAR 2015 AZUNGUMZA NA VIJANA JIJINI MWANZA

Star wa Airtel Trace Music 2015, Mayunga Andrew Nalimi-MAYUNGA, akizungumza na #BMG kuhusiana na project yake ambayo anaifanya na star M-Rap. Na George Binagi-GB Pazzo Project inaitwa Across Lovers and Friend Music Tour ambayo Mayunga anaitumia kukutana na mashabiki zake na kuwapa burudani ikizingatiwa tangu atoke Marekani hakuwahi kufanya tour kama hiyo kwa ajili ya mashabiki zake. Mayunga amesema Project hiyo imeanzia Mwanza na itaendelea katika mikoa mingine na hata nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda, Malawi na Afrika Kusini. Awali Mayunga pamoja na M-Rap kwa kushirikiana na Star Foundation na Kwanza Online na timu nzima ya Trace Music, waliweza kukutana na vijana Jijini Mwanza kwa ajili ya kuzungumza nao kuwahamasisha kutumia vipaji vyao ili kujikwamua kimaisha. Mayunga akizungumza na BMG Stella Mutta ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Star Foundation ya Jijini Mwanza, akizungumza na BMG Petro Malongo ambaye ni mmoja wa Vijana wali...

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANZIBARI BOSTON

Na Mwandishi wetu Boston  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliwasili Zanzibar akitokea Ughaibuni baada ya kukamilisha awamu ya pili ya ziara yake ya Mataifa mbalimbali Ulimwenguni. Wazanzibari wakimsikiliza Maalim Seif ( Picha na swahilivilla.Blog ) Katika awamu hiyo ya pili, Maalim Seif alitembelea Marekani na kupata nafasi ya kuzungumza na Wazanzibari katika jimbo la Massachusetts. Ifuatayo ni sehemu ya mwisho ya mfululizo wa makala zetu za "Maalim Seif azungumza na Wazanzibari Boston" Akiwa mwishoni mwishoni mwa hotuba yake, Mwanasiasa huyo Mkongwe alikariri msimamo wa CUF wa kutoitambua serikali ya Zanzibar iliyoko madarakani kwa vile haikupata ridhaa ya wananchi, akisisitiza kuwa serikali hiyo pia haitambuliki Kimataifa. "Hatuitambui serikali ya Dakta Shein, na hakuna taifa hata moja linaloitambua", alisisitiza. Maalim Seif alielezea kwamba, wakati wa Serikali ya U...

N/WAZIRI JAFO: WATANZANIA WANAPASWA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo. Mgeni na Mwenyeji wakifurahi kufuatia maandalizi mazuri ya Maonesho ya Nane nane kanda ya kati. Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza maelezo ya namna ya kulima kilimo na ufugaji wa kisasa Na Mathias Canal, Dodoma Watanzania wametakiwa kuthamini na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania hususani katika sekta ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi kwani hakuna sababu ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ilihali bidhaa hizo wanazoagiza zinazalishwa na watanzania wenzao. Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said ameyasema hayo mara baada ya kutembelea baadhi ya mabanda katika maonyesho ya wakulima Nane nane Kanda ...

KIJIJI CHA LUDILO WAPITISHA SHERIA NDOGO ZA USIMAMIZI WA MALIASILI

Wananchi wa kijiji cha Ludilo wilayani Mufindi, mkoani Iringa wamepitisha sheria ndogo ya usimamizi wa maliasili (misitu na wanyamapori) ilikukabiliana na kasi ya uharibifu wa rasilimali hizo. Hatua hiyo ilifikiwa tarehe 4 Augusti, 2016 katika mkutano wa hadhara ambapo Diwani wa kata ya Mdabulo Mheshimiwa Henry Nyeho pamoja na Mwanasheria wa Wilaya ya Mufindi Leonard Jaka walihudhuria mkutano huo. Sheria zilizopitishwa na wananchi hao ndio itakayotumika katika usimamizi wa maliasili. Mchakato wa uboreshaji sheria ulianza mwezi Juni, 2016 ambapo Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Mwanasheria wa Wilaya ya Mufindi pamoja na wananchi hao, kupitia mkutano wa hadhara waliangalia upya sheria zilizokuwa zikitumika kijijini hapo na kugundua kuwa zilikuwa na mapungufu.  Wananchi wakiongozwa na Wanasheria kutoka LEAT na Mwanasheria wa Wilaya Mufindi walitoa mapendekezo ya maboresho na kuiruhusu timu ya LEAT...

LHRC YAMPA MAPOKEZI MAKUBWA MWANAHARAKATI GELINE FUKO AKITOKEA MAREKANI

Geline Fuko (kushoto) akipokea maua kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),ikiwa ni ishara ya kumpongeza baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana, akitokea Marekani alikokuwa akihudhuria mafunzo ya vijana wa kiafrika yaliyoandaliwa na  Rais Obama.  Na Dotto Mwaibale SHANGWE ilitawala wakati mtanzania Geline Fuko alipo wasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa nne usiku jana Agosti 5, 2016 akitokea nchini Marekani alikohudhuria mafunzo ya viongozi vijana kutoka Bara la Afrika.  Wafanyakaziwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao ni wafanyakazi wenzake wa Geline, familia ya Geline, ndugu na marafiki walitoa mapokezi ya kishujaa wa wanaharakati huyo aliyetajwa kuwa mfano wa kuigwa na Rais Obama. Akizungumza na wanahabari, Geline alisema amefarijika na hakutarajia kama wazo lake la kuanzishwa kwa Kanzidata ya K...