Skip to main content

Posts

Showing posts from March 2, 2012

Mratibu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) : PUNGUZENI KASI YA MAAMBUKIZI

SONGEA Mratibu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Petro amesema kuwa ili kupunguza kasi ya maambukizo ya Virusi Vya Ukimwi mkoani hapa halmashauri na wadau wengine wa Ukimwi hazina budi kufanya kazi kwa pamoja. Alisema kuwa ili kufanikisha mkakati wa taifa wa kinga dhidi ya VVU halmashauri na wadau wengine wanapaswa kufanya kazi kwa karibu na hatimaye kuweza kupunguza maambukizo haya. Mratibu TACAIDS (M) huyo alitoa rai jana katika kikao cha kupitia mipango ya shughuli za Ukimwi za Halmashauri kilichofanyika Peramiho kikihusisha Waratibu wa Ukimwi Kinga Wilaya (CHAC) na Waratibu wa Ukimwi-Tiba katika ngazi ya wilaya yaani (DACC) wa kutoka Halmashauri zote za Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma yaani Songea Manispaa, Songea Vijijini, Namtumbo, Mbinga na Tunduru. Alisema kuwa  lengo la kikao hicho cha siku mbili ni kupima shughuli za Ukimwi za halmashauri  kama zinaendana na miongozo ya kitaifa,kama ...