Skip to main content

Posts

Showing posts from October 9, 2015

When to Tell People You're Pregnant

Question: "I'm a healthy 20-something on my first pregnancy, and I'm just itching to tell people I'm expecting. When should you tell people you're pregnant — do you really have to wait until your second trimester to share?" 22 shares TRENDING WITH MOMS First Year The Steps Hospitals Should be Taking for Breastfeeding Moms Family One More Reason to Love New Dad Justin Timberlake Pregnancy How Much is Your Baby's Name Worth? Congratulations on the big news! It's really tough to keep this secret when you just want to shout from the nearest rooftop, "I'm having a baby!" Most moms-to-be do wait to  share their news until after week 13 of pregnancy, when the rate of miscarriage goes way down. But that doesn't mean you have to. Consider that healthy women start off with a lower  rate of miscarriage  than other moms-to-be since they're not as vulnerable to the infections...

MAGAZETI LEO JUMAMOSI

NEC KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUHAKIKISHA AMANI INATAWALA SIKU YA UCHAGUZI

Jaji Mstaafu Damiani Lubuva  Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi kutoruhusu vikundi vya watu karibu na vituo vya kupiga kura kwa madai ya kulinda kura. Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa mkutano wa tume na wasimamizi wa uchaguzi wakiwemo makamanda wa polisi wa mikoa nchini. Jaji Lubuva ameeleza lengo la mkutano huo uliofanyika jana, ni kujadili na kupeana uzoefu juu ya wajibu na taratibu za mchakato wa uchaguzi kuanzia sasa mpaka hapo muda wa kutangaza matokeo. Pamoja na hayo kiongozi huyo wa NEC amewataka washiriki wa kikao hicho kuzingaia maadili na kusimamia makubaliano yatakaofikiwa katika mkutano huo. Zimebaki siku 16 kufikia uchaguzi mkuu mwaka huu na tayari tume ya uchaguzi imeshakutana na makundi mbalimbali ya wananchi kuelezea maendeleo na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na tume hiyo katika kuhakikisha kuwa ucha...

MARAIS WASTAAFU KUTOKA AFRIKA WAJA KUONGOZA UFUATILIAJI WA UCHAGUZI...

Marais wastaafu wawili kutoka Afrika, watakuwa miongoni mwa waangalizi wa kimataifa watakao kuepo Nchini kuangalia Jinsi Uchaguzi mkuu utakavyo endeshwa Tarehe 25 Oktoba. Hawa ni Rais mstaafu Goodluck Jonathan wa Nigeria ambaye ataongoza timu ya waangalizi upande wa Jumuia ya Madola na kiongozi wa zamani wa Mozambique Armando Guebuza ambaye ataiongoza timu ya waangaliaji upande wa Umoja wa Afrika. Ujio wao ulibainishwa jana,wakati wizara ya mambo nje,ushirikiano wa kimataifa na umoja wa mataifa walipo toa taarifa kwenye vyombo vya habari ku washiria miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Timu za Jumuia ya madola na Umoja wa Afrika watakuwa miongoni wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25,waangalizi wengine ni kutoka Jumui ya Ulaya na SADC. Huu ni uchaguzi Mkuu wenye wafuatiliaji wengi kutoka Nchi za nje .

Mrema, Dk Magufuli wapigiana kampeni Vunjo

Katika hali ambayo haikutarajiwa Mwenyekiti wa TLP taifa, Augustino Mrema jana amemnadi mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli kuwa ndiye anafaa kuwa Rais wakati chama chake kikiwa kimemsimamisha, Macmillian Lyimo kuwania nafasi hiyo ya Urais kwa tiketi ya TLP. Hali hiyo ilianza kwa Dk Magufuli kumpigia debe Mrema anayewania ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP kwa kusema kuwa ana historia nzuri na uzoefu katika uongozi kuliko wengine. Dk Magufuli alisema hayo jana wakati akihutubia wananchi katika uwanja wa polisi Himo ambapo alisema wananchi wasikosee kwenye kupiga kura na kuwa hatakama hawaitaki CCM, basi wampigie kura Mrema.

BBC Walivyomuelezea Lowassa

Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika ya jamii ya wafugaji Kaskazini mwa Tanzania.Alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha. Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza (1983-1984). Uzoefu katika siasa Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi. Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni. Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa 1977. Kabla ya kugombea ubunge , aliwahi kutumikia jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd Amin kuondolewa madarakani. Baada ya hapo alikuwa mtumishi wa umma kwa miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa mbunge kuwajilisha vijana na kujiunga rasmi na siasa. Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la uchagu...

COSATO CHUMI AKERWA PROGANDA CHAFU ZINAZOFANYWA NA MPINZANI WAKE!

Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi (CCM) (katikati) akielezea masikitiko yake kuhusu kutoridhishwa na kampeni na propaganda chafu zinazofanywa na mgombea mwenzangu wa Chadema kwa waandsihi wa habari jana. Kushoto ni Meneja wa Kampeni -Jimbo la Mafinga mjini Albert Chalamira na Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Mufindi, Nuru Ngeleja (kulia) Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa mgombea na waandishi wa habari katika ofisi za chama mjini Mafinga jana Meneja wa Kampeni -Jimbo la Mafinga mjini Albert Chalamira (katikati) akielezea hali kampeni katika jimbo hilo kwa wanahabari ambapo alisema kuwa CCM inauhakika wa kushinda uchaguzi kwa asilimia 80. Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi (CCM) akionesha waraka wa kampeni chafu zinazodaiwa kumuzoofisha iliyopewa jina MKAKATI WA USHINDI JIMBO LA MAFINGA MIJINI kwa wanahabari. (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA) Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) amesema ni jambo ...

MAADHIMISHO YA MIAKA 70 YA UN NCHINI TANZANIA KUFANYIKA OKTOBA

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta kabisa umaskini.(Picha zote ne Geofrey Adroph wa Pamoja Blog). Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa yatakayofanyika siku ya Jumanne Tarehe 13, Oktoba katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez. Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiendelea kufuatilia yanayojiri kwenye mkutanoni na waandishi wa habari. Waandishi wa habari wakif...