Posted by Ngabwe Mlulu on 08:31 Amina Kisenge Na Dotto Mwaibale WALIMU wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaidai Serikali jumla ya sh. Bilioni 1.1 za madai yao mbalimbali kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015. Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dar es Salaam, Mwalimu Amina Kisenge (pichani kushoto), katika kikao cha baraza la dharura la chama hicho lililoketi hivi karibuni. Awali CWT ilikua ikidai jumla ya Sh.Bilioni 3.9 kabla ya kupunguza kiasi cha Sh.Bilioni 1.9 mapema mwaka huu. Kwa mujibu wa Mwenyekiti, madeni hayo ni pamoja na malimbikizo ya nauri za likizo kuanzia mwezi wa Juni na Desemba, 2013; na Juni na Desemba mwaka jana. Malimbikizo mengine ni pamoja na pesa ya kuwasafirisha wastaafu kwenda majumbani kwao, alisema Kisenge. "Uhamisho wa walimu kutoa kituo kimoja kwenda kingine ikiwa ni posho ya usumbufu na ya kujikimu; pamoja na pesa za gharama za masomo baada ya walimu kujigharamia kuji...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.