TIMU ya Abasia Peramiho FC jana waliitafuna Abasia Hanga FC mabao 2-0, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa Hanga Wilayani Namtumbo, Mkoani Ruvuma. Timu hizo zote mbili ni za watawa ambapo Abasia Peramiho ni wa ‘Benedictine White Fathers’ wa Peramiho ya Wilaya Songea (V) na Abasia Hanga ni ya ‘African Benedictine Fathers’ wa Hanga wilayani Namtumbo., Mkoani Ruvuma. Katika mechi hiyo, Abasia Peramiho ilingia kwa nguvu na kupeleka mashambulizi mfululizo na kufanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika chache za mwanzo kipindi cha kwanza, lilofungwa na Davis Komba baada ya kupata klosi kutoka kwa winga wa kulia wa timu hiyo. Kama hivyo haitoshi, Abasia Peramiho waliaandika bao la pili kwa kupata penati baada ya mabeki wa Timu ya Hanga kumuangusha mshambuliaji wa Abasia Peramiho, Bro.Jerome katika eneo la hatari, na Mwamuzi Bro. Deogratias Komba kutoka Peramiho kuwazawadia penati. Bada ya kufungwa mabao hayo, Hanga FC ilitulia na kuanza kupeleka mashambulizi langoni mwa ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.