Skip to main content

Posts

Showing posts from December 17, 2016

MBUNGE KAFULILA ARUDI CHADEMA

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila leo ametangaza kukihama chama hicho na kusema kuwa atajiunga na Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA). Kafulila ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika bunge la kumi kwa kufichua hoja mbalimbali za ufisadi amesema kuwa ameshawasilisha barua ya kujiuzulu kwa uongozi wa chama hicho. Akieleza sababu iliyomsukuma kujiunga na CHADEMA, Kafulila alinukuliwa akisema kuwa kikubwa ni kuhakikia wanaleta mabadiliko nchini Tanzania.  "Ili kufanya safari kuwa fupi, kuondoa vikwazo vya huyu yuko chama hiki mwingine kile nimeamua kujiunga na CHADEMA ili kurahisisha uletaji mabadiliko katika nchi yetu sababu nimeona uhitaji huo," alisema Kafulila. Katika uchaguzi uliopita Kafulila alipoteza jimbo la Kigoma Kusini ambalo lilikwenda wa Hasna Sudi Katunda Mwilima aliyekuwa akigombea kupitia Chama cha Mapinduzi.

MMILIKI WA JAMIIFORUM AENDELEA KUSOTA LUMANDE

Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo akiongozwa na Askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo, kusomewa mashtaka yanayomkabili kama inavyosomeka hapa chini. Mwanzilishi-mwenza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence MeloMubyazi (40), leo amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana katika kesi moja kati ya tatu zinazomkabili ikiwamo ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuendesha mtandao wa Jamii Forum bila usajili. Mapema leo asubuhi mshtakiwa huyo ambaye pia ni mfanyabiashara na bosi wa mtandao huo, alifikishwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mapema asubuhi. Alipandishwa kizimbani saa 3:29 kusomewa mashtaka katika kesi yake ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Upande wa mashtaka uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mohamed Salum akisaidiana na Wakili wa Seri...

SERIKALI YAWATOA HUFU WANANCHI KUHUSU UGONJWA WA ZIKA,SOMA HAPO KUJUA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha uwepo wa taarifa juu ya ugonjwa wa ZIKA hapa nchini. Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dk. Hamisi Kigwangalla wakitolea ufafanuzi mbele ya waandishi wa Habari, wamesema wananchi wasiogope na wamewatoa hofu kwani taarifa zilizotolewa awali na kuripotiwa na vyombo vya habari walizonukuu kutoka NIMR hazina ukweli wowote na za kupuuzwa. Aidha, kwa mujibu wa Kaimu Mkuu kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Afya), Bi. Catherine Sungurakatika taarifa ya Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu ilieleza: “Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Zika nchini. Kama nilivyoeleza mnamo tarehe 31 Januari 2016, ugonjwa huu bado haujaingia nchini, na leo pia napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa Tanzania haujathibitishwa kuwepo na ugonjwa wa Zika. Utafiti uliofanywa na NIMR, ulikuwa ni utafiti ...