Skip to main content

Posts

Showing posts from March 27, 2026

RC Kheri James: Waziri Mkuu Kuongoza Waombolezaji Mazishi ya Kitaifa ya William Lukuvi

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, atawaongoza waombolezaji katika mazishi ya kitaifa ya marehemu William Lukuvi. RC James pia ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mazishi hayo, akisisitiza kuwa ni tukio muhimu la kitaifa la kumuaga kiongozi aliyelitumikia taifa kwa muda mrefu. Marehemu William Lukuvi aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu wenye Ulemavu). Akizungumza leo na waandishi wa habari wakati akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu kilichopo Mtaa wa Lukuvi, Kata ya Gangilonga, Manispaa ya Iringa, Kheri James alisema serikali imeandaa mazishi hayo kwa hadhi ya kitaifa na inatarajia ushiriki mkubwa wa waombolezaji. Aliongeza kuwa mazishi hayo yatafanyika katika Kijiji cha Idodi, Jimbo la Isimani, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo viongozi mbalimbali waliopo madarakani pamoja na waliostaafu wanatarajiwa...

Lukuvi Aacha Alama Isiyofutika Isimani, Wanafunzi wa Shule Yake Wamkumbuka kwa Moyo wa Shukrani

  Iringa. Marehemu William Lukuvi, aliyewahi kuwa Waziri na Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa, anakumbukwa kama kiongozi mwenye moyo wa kujitolea, aliyeacha alama isiyofutika katika maisha ya wananchi na maendeleo ya jamii.   Ndani na nje ya siasa, Lukuvi alijijengea heshima kutokana na misingi yake ya haki, usawa na upendo kwa watu, hali iliyomfanya kupendwa na kuaminiwa na makundi mbalimbali ya jamii.   Kwa mujibu wa Thom Lukuvi, aliyemtaja marehemu kama “baba mdogo,” familia inamkumbuka kama nguzo muhimu iliyodumisha mshikamano na ustawi wa ukoo. Alisema marehemu hakuwa tu kiongozi wa kisiasa bali pia mlezi na mshauri aliyekuwa tayari kusaidia mtu yeyote aliyehitaji msaada.   “Alikuwa mtu wa watu, hakubagua. Alisikiliza changamoto za kila mmoja na kujitahidi kuzitatua kadri ya uwezo wake,” alisema Thom.   Aliongeza kuwa pale ambapo hakuwa na uwezo wa kusaidia, Lukuvi hakutoa ahadi zisizotekelezeka bali alichagua kusema ukweli, jambo lil...

Lukuvi Leaves a Lasting Legacy in Isimani, Students at His School Remember Him with Gratitude

Iringa. The late William Lukuvi, who served as a Minister and Member of Parliament for Isimani Constituency in Iringa Region, is remembered as a dedicated leader who left an indelible mark on the lives of the people and the development of the community. Both in and out of politics, Lukuvi earned respect for his strong principles of justice, equality, and compassion, which made him widely loved and trusted by different groups in society. According to Thom Lukuvi, who described the deceased as a “young father,” the family remembers him as a key pillar who upheld unity and the well-being of the extended family. He said the late leader was not only a political figure but also a guardian and advisor who was always ready to help those in need. “He was a man of the people; he never discriminated. He listened to everyone’s challenges and did his best to resolve them within his capacity,” said Thom. He added that whenever he was unable to assist, Lukuvi would not make unrealistic promis...