Kufuatia serikali kupitisha muswada wa ongezeko la VAT kwa watalii ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali, MO Blog imepata nafasi ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Travel Partner, Erick Mashauri ili kujua ni kwa kiasi gani ongezeko hilo limeathiri biashara kwa makampuni yanayopeleka watalii mbugani na kwa sekta ya utalii kwa ujumla. Mashauri alisema kuwa ongezeko la VAT kwa watalii limeathiri kwa kiasi kikubwa biashara zao kwani serikali ilifanya maamuzi ya haraka bila kuangalia athari ambazo zingejitokeza baada ya kupitisha muswada na haikuwashirikisha wao kama wadau wa karibu ambao wanafanya biashara ya kuwahudumia watalii wawapo nchini. "Ongezeko la VAT ambalo serikali ilifanya limevuruga biashara ya utalii, ilisahau kama wageni hawa huwa wanafanya booking mwezi mmoja kabla ya safari, tukashangaa serikali inapeleka muswada haraka haraka bungeni na kuupitisha bila kuangali athari ambazo zitajitokeza, ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.