Skip to main content

Posts

Showing posts from January 13, 2017

HALMASHAURI YAIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA SHULE YA MSINGI HAZINA MISION ...

Na Woinde Shizza,Arusha HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya  msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa mara baada ya uongozi wa shule  hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza watumishi  wake pamoja na mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika  uandikishaji wa shule. Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja mara baada siku chache  zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa  kuwalipa mishahara watumishi na walimu wa shule hiyo na hivyo kutakiwa  kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya  maagizo hayo kwa muda waliopewa. Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo kaimu afisa elimu shule za  msingi katika jiji la arusha Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua  kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya  marekebisho waliyotakiwa k...

WANAFUNZI 17,549 KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI MKOANI IRINGA

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (kushoto) ambaye pia ni Katibu wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa (RCC) akisoma taarifa katika kikao hicho huku Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye pia mwenyekiti wa kikao hicho akifuatilia kwa makini leo.  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Suzana Mgonukulima (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, Menrad Kigola (CCM) wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa Iringa (RCC kilichofanyika leo  (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA) IRINGA: Jumla la wanafunzi 17,549 mkoani Iringa (wavulana 7,988 na wasichana 9,561) sawa na mkiondo 439 watajiunga kidato cha kwanza mwaka 2017, imeelezwa. Hayo yalisemwa na Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa Richard Mfugale (pichani) wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika leo mjini Iringa. Kaimu afisa elimu huyo alisema kuwa wanafunzi wote waliofauli wam...

SIASA ZA CHUKI NA CHAFU HAZIWEZI KULETA MAENDELEO KATIKA TAIFA LETU

Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhandisi Shaban Kaswaka (kushoto), akimtambulisha kwa wananchi Mgombea Udiwani kupitia chama hicho Kata ya Kijichi, Abdallah Shamas katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Temeke jijini Dar es Salaam jana. Wafuasi wa CUF wakimkaribisha mgombea udiwani wa Kata ya Kijichi wakati alipokuwa amewasili kwenye mkutano wake wa kampeni. Meza kuu katika mkutano huo. Mkutano ukiendelea. Wafuasi wa chama cha CUF wakiinua mikono kukubali kumpigia kura mgombea wa chama hicho. Na Dotto Mwaibale MGOMBEA Udiwani Kata ya Kijichi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Khalid Shamas amewataka wananchi na wagombea wenzake kuacha siasa za chuki na chafu ili kuiletea maendeleo kata hiyo na taifa kwa ujumla. Shamas alitoa ombi hilo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Kijichi Dar es Salaam jana wakati aki...