Na Woinde Shizza,Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo. Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali. Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu wachache...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.