Iringa. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameomba wananchi wa kata ya Lyamgungwe, Wilaya ya Iringa, kumpa tena ridhaa ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu. Akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wakati wa kampeni, mgombea huyo alisema kipindi cha miaka mitano iliyopita kilikuwa cha kujifunza, huku akieleza kuwa endapo atapewa nafasi nyingine, ataendeleza miradi ya maendeleo aliyoianzisha. Alibainisha kuwa moja ya changamoto zinazowakabili wananchi ni ukosefu wa vyumba vya kuhifadhi maiti katika vituo vya afya, na kuahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha kila kituo kinakuwa na huduma hiyo ili kupunguza gharama za kupeleka maiti katika Hospitali ya Tosamaganga. Aidha, alitaja mafanikio aliyoyapata katika kipindi chake cha ubunge ikiwemo kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mgama, hatua ambayo imesaidia kurahisisha usafirishaji wa mazao na huduma muhimu. “Chama Ch...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.