Skip to main content

Posts

Showing posts from August 21, 2015

WAGOMBEA RASMI WA URAIS NI 8 TU, WENGINE HAWAJAKIDHI VIGEZO.

Hatimaye katika vyama 12 vilivyochukua fomu za kugombea urais, ni vyama 8 tu ambavyo wagombea wake wamekidhi vigezo vya kugombea urais mwaka huu Tanzania. Vyama hivyo ni CCM, CHADEMA, TLD, ADC, CHAUMA, ACT- WAZALENDO, NRA na UPDP. Wagombea hao 8 na vyama vyao ni 1. John Magufuli (CCM) 2. Edward Lowassa (CHADEMA) 2. Anna Mghwira (ACT) 4. Fahmi Dovutwa (UPDP) 5. Chifu Lutalosa Yemba (ADC) 6. Janken Kasambala (NRA) 7. Hashim Rungwe (CHAUMA) 8. macmillan lyimo (TLP) Wagombea wa vyama vitatu hawajakidhi vigezo vya kugombea urais wa Tanzania, vyama hivyo ni CCK, DP , TADEA.. Chama cha AFP chenyewe hakijafika kabisa katika ofisi za NEC kuleta fomu zake.

NEC YAMTEUA LOWASSA NA MGOMBEA MWENZA WAKE, JUMA DUNI HAJI, KUWA WAGOMBEA RASMI WA URAIS WA TANZANIA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi, Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa Kampeni, kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara b...