Skip to main content

Posts

Showing posts from November 22, 2012

ZAIDI YA WAGONJWA 80 WAMEPATIKANA NA MTOTO WA JICHO MKOANI RUVUMA

Na Friday Simbaya, Songea Hospitali ya Peramiho ya Mt. Josefu kwa kushirikiana na daktari bingwa wa macho Dr. Grasbon toka Ujerumani waliendesha kambi ndogo ya macho, ambapo ilianza tarehe 5-12/11/2012. Kambi hiyo ya macho ilifanikiwa kuona wagonjwa zaidi ya 120 toka sehemu mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma, ambapo wagonjwa 80 walipatikana na ugonjwa wa mtoto wa jicho (Cataract). Akizungumza na Gazeti la Mwenge hivi karibuni Dr. Wade Kabuka ambaye ni daktari wa macho katika Hospitali ya Peramiho, amesema tatizo la macho katika mkoa wa Ruvuma lipo na wagonjwa ni wengi. Amesema kuwa wakati wakiendesha kambi ya upimaji wa macho kwa ufadhili wa hospitali ya Peramiho kwa kushirikiana na Dr. Grasbon toka Ujerumani, wagonjwa waliojitokeza ni wengi sana, na wengi wao walikuwa na matatizo ya mtoto wa jicho. Amesema kuwa zaidi ya wagonjwa 120 walipimwa na kati yao 80 waligundulika na tatizo la mtoto wa jicho (Cataract), ambapo wote walipata matibabu kwa kuwekewa kioo ndani ya jicho. “Ugo...