Kilolo, Iringa – Septemba 14, 2025 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC) na Mratibu wa Kampeni Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Salim Abri maarufu kama Asas, leo amezindua rasmi kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilolo pamoja na wagombea wa nafasi za udiwani kupitia CCM katika jimbo hilo. Mgombea Ubunge wa Kilolo, Dr. Ritta Kabati, ndiye mwanamke pekee kati ya wagombea wa majimbo saba ya ubunge mkoani Iringa kupitia CCM. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dr. Kabati aliishukuru CCM kwa kuendelea kumuamini na kumpa jukumu la kupeperusha bendera ya chama, akisisitiza kuwa uzoefu wake wa miaka 15 kama Mbunge wa Viti Maalum umemwandaa vyema kuwatumikia wananchi wa Kilolo kwa bidii, uadilifu na upendo. Ameahidi kutekeleza kikamilifu Ilani ya CCM 2025–2030 bila upendeleo, huku akihimiza mshikamano kati ya viongozi na wananchi, kuvunja makundi ya kijamii na kisiasa, na kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo. Aliwaomba wananchi kumpigia kura yeye, Rais Samia Suluhu Hassan na madiwani w...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.