Skip to main content

Posts

Showing posts from December 16, 2010

UCHAWI NA MAJINI NINI?

  Mwandishi wa kitabu kidogo cha Uchawi na Majini Nini? Padre Geogory Mwageni OSB ana kwa ana na mmliki wa blog hii akipitia baadhi ya vitabu alivyoandika leo katika Duka la Vitabu la Peramiho, Songea mkoani Ruvuma. Kitabu hicho kilichapishwa na Benedictine Publication Ndanda-Peramiho. Pata nakala yako sasa iliujue kwa undani masuala ya uchawi na majini kama kunahusiano au la. " Nimezaliwa Ubena mnamo mwaka 1922 wakati jamaa zangu wote walipokuwa wapagani. Nilijifunza dini ya kikristo, shuleni tu. Mwaka 1935 niliingia seminari ndogo ya Peramiho, Ungoni. Baadaye nikaishi Kigonsera, tena Peramiho, mwishowe nikaingia utawa Liganga. Tangu kupata upadre mwaka 1954 hadi kuingia utawa nalihudumia katika Umatengo. Tangu 1960 naishi Hanga katika nchi ya Undendeule katika Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma"

PRESIDENT KIKWETE AT THE GREAT LAKES SUMMIT IN LUSAKA ZAMBAIA

President   Dr. Jakaya Mrisho   Kikwete in conversation with the UN Deputy Secretary General Dr.Asha Rose Migiro in Lusaka during the just ended Special summit on The Fight of   illegal exploitation of natural resources.   President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete consults with the Deputy Minister for Minerals and Energy Adam Kighoma Malima during the opening session of the special summit on the fight of Illegal exploitation of Natural resources held in Lusaka Zambia yesterday.On the left partially seen behind the president is the deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Mahadhi Juma Maalim. Zambian President Rupiah Bwezani Banda in conversation with the Executive Secretary for the International Conference on the Great Lakes Region Ambassador Liberata Mulamula during the opening session of the special Summit on the Fight of Illegal Exploitation of Natural Resources in Lusaka Zambia yesterday. COURSEY OF IKULU MAWASILIANO

MADIWANI SIMAMIENI UTUNZAJI MAZINGIRA- DR. HOVISA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa amewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kusimamia kwa karibu sana masaula ya utunzaji mazingira katika kata zao zote, kwa kuwa uharibufu wa mazingira ni tatizo la dunia nzima na kuongeza kuwa tunakoelekea ni kubaya zaidi kwa kuwa madhara ya uharibifu wa mazingira yanaonekana zaidi katika jamii. Hayo yalisemwa na waziri wa mazingira huyo alipokuwa akizungumza na madiwani walipokuwa katika kikao cha kamati cha madiwani kilichofanyika Songea mjini katika Ukumbi wa Tumbaku (NGOMATI). Waziri huyo alisema kwamba atahakikisha na atasimamia kwa nguvu na juhudi zake zote suala la uharibifu wa mazingira na hivyo madiwani wahamasishe wananchi katika maeneo yao wanakotoka. Aliwataka madiwani hao kuwashauri wananchi wao ambayo sehemu kubwa ni wakulima wadogo wadogo kwamba tabia ya kukata miti yote katika mashamba yao wakati wa kulima na kufanya palizi basi watunze miti kadhaa katika masha...