Skip to main content

Posts

Showing posts from March 6, 2026

RC Kheri James Awataka Wafanyabiashara Kufuata Maeneo Waliyopangiwa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, leo Ijumaa Machi 6, 2026 amewataka wafanyabiashara kufanya biashara katika maeneo rasmi waliyopangiwa ili kusaidia kuweka miji katika mpangilio mzuri na kuepusha msongamano usio wa lazima. RC James alitoa kauli hiyo wakati akifunga kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika mkoani Iringa. Katika kikao hicho pia alipangua hoja ya baadhi ya wajumbe waliopendekeza Iringa kupandishwa hadhi na kuwa jiji, akisema bado kuna masuala ya msingi yanayohitaji kufanyiwa kazi kabla ya kufikia hatua hiyo. Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha miundombinu, mipango miji na huduma za kijamii ili kuhakikisha mkoa unakuwa katika mpangilio unaokidhi vigezo vya kuwa jiji. Wakati huo huo, Mbunge wa Kilolo Ritta Kabati pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Fadhili Ngajilo walitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu namna ya kuwasaidia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga kufanya biashara zao katika mazingira bora bila kuathiri mpangilio wa miji. ...