Mbeya: Mkurugenzi na kiongozi wa taasisi ya dini ya Daily Bread Life Ministry Tanzania, Mchungaji James Mpeli Mwaisumbe amewasihi watanzania kumuombea Rais Dkt John Pombe Magufuli ili aweze kuliongoza taifa kwa haki, amani na upendo. Alisema kuwa ili Tanzania iweze kusonga mbele, waislamu, wakristo,viongozi wa siasa, serikali na watanzania kwa ujumla lazima waliombee taifa na viongozi wake kwa Mungu ili kuweza kudumisha amani na mshikamano viliyopo. Mchungaji Mpeli alisema hayo wakati wa sherehe ya kumuaga Mchungaji Raphael Mwasifiga wa Kanisa la Baptist, Kanani lililopo Sinde Makunguru, Mwanjelwa jijini Mbeya. Mchungaji huyo mwalikwa alisema kuwa anavutiwa na kiongozi wa nchi kwa sababu ni mcha Mungu na katika maneo yake kumi anayozungumza hakosi kumtaja Mungu. Alisema kuwa taifa ni kitu cha muhimu kuliko vya vyama siasa na kuwaomba wakristo, waislamu viongozi wa siasa na serikali kuliombea taifa ili amani na mshikamano ambayo havipatikani Afrika i...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.