Skip to main content

Posts

Showing posts from January 23, 2017

Mwenyekiti wa Chadema apewa siku 14 awe amelipa kodi

Miezi takribani mitano iliyopita tangu aondolewe Billcanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame Mkoani Kilimanjaro. Uamuzi huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro,umefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile kilichosema lipo ndani ya chanzo cha maji. Byakanwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM). “Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza ku...

WAUMINI WAAMUA KUMZUIA KANISANI ASKOFU MOKIWA

Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam wa Kanisa la Anglikana, Dk valentino Mokiwa jana alishindwa kuendesha vikao viwili baada ya kundi la waumini kufika Usharika wa Ilala kwa lengo la kuzuia. Askofu Mokiwa, ambaye anapinga uamuzi wa Askofu Mkuu wa Anglikana, Dk Jacob Chimeledya kumvua madaraka kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, alikuwa aendeshe vikao vya kamati ya fedha na halmashauri kuu, lakini alilazimika kuviahirisha baada ya kundi hilo kufika eneo hilo. Wakati waumini hao wakizuia vikao hivyo kufanyika, mashemasi, mapadri, wainjilisti na waumini wa dayosisi hiyo wametoa tamko la kumuunga mkono Dk Mokiwa wakipinga uamuzi wa mkuu wa kanisa hilo kumvua madaraka. Askofu Mokiwa anapinga uamuzi wa kumvua madaraka akisema hauwezi kufanywa na mkuu wa kanisa, bali na halmashauri kuu ya jimbo ambayo anasema haikushirikishwa zaidi ya kutaarifiwa uamuzi huo. Tukio la jana la kumzuia Dk Mokiwa kufanya mkutano lilitokea saa mbili asubuhi katika Kanisa l...

ASKOFU MDEGELLA WA KKKT IRINGA AAGWA KWA KUZAWADIWA NYUMBA NA GARI

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, Isaya Mengele (kushoto) akimpongeza Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella katika ibada maalum iliyofanyika katika usharika wa Kanisa Kuu (Cathedral) Iringa mjini leo. (Picha na Friday Simbaya ) KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa limemzawadia Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella aliyemaliza muda wake wa uaskofu nyumba na gari vyenye thamani ya shilingi milioni 123. (123m/-). Kanisa limeamua kumzawadia nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 55/- iliyopo katika mtaa wa Kihesa-Kilolo Manispaa ya Iringa na gari aina ya Toyota Haice Pickup double cabin yenye thamani ya shilingi milioni 68/-. Askofu Mdegella alizaliwa mwaka 1951 katika Kijiji cha Ipalamwa, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.  Askofu huyo amekuwa askofu mkuu wa dayosisi ya Iringa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa miaka 38 kama mchungaji, na miaka 30 kama askofu . Askofu...