Skip to main content

Posts

Showing posts from October 7, 2017

PSPF YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE KWENYE KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia wateja, (wanachama) wa Mfuko. Bw. Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017. Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja. "Wakati nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu." Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam.  Bw. May...