Skip to main content

Posts

Showing posts from July 25, 2011

WAKAZI WA LUNDUSI

Wakazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea, Mkoani Ruvuma wakisaidiana Bi. Clementina Mlowe (mwenye Khanga nyekundi na kilemba)kupukuchua na kujaza mahindi kwenye mifuko. Mkazi huyo wa Lundusi amebahatika kuvuna gunia 80 za mahindi.

BUMPER HARVEST IN RUVUMA REGION

Na Friday Simbaya, Songea Wakati mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mvua za masika na vuli kutonyesha vizuri katika msimu wa kilimo mwaka huu, Mkoa wa Ruvuma unasemekana kuwa na chakula cha ziada kutokana na mavuno mzuri ya chakula msimu huu. Wakati huohuo, wakazi wa vijiji vya Lundusi na Maposeni Wilayani Songea Mkoani Ruvuma wameipongeza serikali kwa mpango kabambe wake wa ‘Kilimo Kwanza’ wa vocha ya ruzuku ya pembejeo uliyowapelekea wananchi wengi kupata mavuno kabambe katika msimu wa mavuno ya mwaka huu. Wakiongea na Nipashe jana katika nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa ni jambo la busara sana kwa serikali kwa kuwawezesha wakulima kupata mavuno mazuri msimu huu kutokana na mkakati mzuri wa vocha za ruzuku ya pembejeo. Walisema kuwa katika maeneo mengi wa Mkoa wa Ruvuma, wakulima wamepata mavuno ya chakula mazuri hasa mahindi, kwa kutumia vyema mvua za masika na zile za vuli, zilizonyesha vizuri msimu huu. Katika kuhakikis...