MGOMBEA nafasi ya Uenyekiti katika Klabu ya soka ya Lipuli Fc 'Wanapaluhengo, Abinery Mrema (kushoto) amewaahidi wanachama na wapenzi wa soka mkoani hapa atahakikisha timu hiyo inamiliki uwanja wa mazoezi endapo atachaguliwa. Wagombea wengine ni Ramadhani Mahani na Nuhu Muyinga. Akizungumza na wanahabari SIMBAYABLOG leo, Mrema alisema kuwa timu ya Lipuli ambayo kwa sasa iko ligi kuu Tanzania Bara haina budi kuondokana na viwanja vya kuazima kwa ajili ya kufanyia mazoezi hivyo atahakikisha timu hiyo inapata uwanja wake. Alisema kuwa licha ya kuwa uwanja wa mazoezi atahakikisha inawekeza katika vitega uchumi ambavyo ni kuwa na kiwanja kwa ajili ya uwekezaji, kuwa na chuo cha mafunzo kwa watoto, na kuhakikisha timu hiyo inapata usafiri wa uhakika. Aliongeza kuwa atahakikisha wanafungua matawi ya timu ya Lipuli nchi nzima na nje ya nchi ambapo watachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa timu ya Lipuli . "Nitahakikisha timu ya Lipuli inakuwa na matawi ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.