Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri (katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog ). Na Andrew Chale, Modewjiblog [DAR ES SALAAM-TANZANIA] Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao. Hayo yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya Wa...