Skip to main content

Posts

Showing posts from August 1, 2010

CCM KURA ZA MAONI

Tawi la Idunda katika Kata ya Mtwivilla, Manispaa ya Iringa katika harakati za kupiga kura za maoni ndani ya CCM ilikuwapata mbunge na diwani leo.

WALIMU WAKOPESHWA PIKIPIKI

Pikipiki zikiwa nje ya ofisi ya SACCOS ya walimu mjini Iringa. Na Friday Simbaya, Iringa CHAMA cha Ushirika cha Akiba na Kukopa cha Walimu wa Iringa Vijini na Kilolo (IRTS-SACCOS LTD) kimekabidhi pikipiki kwa walimu wanachama 19 katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya chama hicho jana. Pikipiki hizo 19, zilitolewa kwa walimu 19 kati ya 27 walikubaliwa kupewa na juhudi zaidi zinafanyika kupata pikipiki nyingine nane (8) zilizobaki ili walimu hao nao waweze kupewa mapema. Akikabidhi pikipiki kwa walimu, Afisa Elimu wa Wilaya shule za msingi (DEO), William Mkagwa, kwa niaba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa (DED), Tina Sekambo, alisema kuwa amefurahishwa na juhudi za SACCOS ya kutatua matatizo ya usafari kwa walimu wanachama kwa kutoa mikopo ya pikipiki ambazo zitarahisisha sana usafari kutokana na hali ya jiografia ya Wilaya. Aidha, Sekambo alishauri pia utaratibu wa mikopo ya vyombo hivi uwe endelevu ili hatimaye walimu wote waweze kupata vyombo hivi. “N...

MWENGE WAINGIA MKOANI IRINGA

Na. Friday Simbaya, Ludewa JUMLA ya miradi sabini na moja (71) yenye thamani ya shilingi 8,369,893,729 itakaguliwa, kuzinduliwa, itafunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi mkoani Iringa kwa mwaka 2010 wakati wa mbio za mwenge. Taarifa hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa Iringa Bibi. Gertrude Mpaka juzi wakati akisoma taarifa fupi ya mkoa wa Iringa wakati wa kupokea mwenge wa uhuru mwaka 2010 katika kijiji cha Kipingu, kata ya Manda wilayani Ludewa ukitokea mkoani Ruvuma. Bi.Mpaka alisema miongoni mwa fedha hizo, shilingi 2,890,484,593 ni fedha toka Serikali kuu, shilingi 951,705,586 ni michango ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa, thamani ya nguvu kazi ya wananchi ni shilingi 1,557,402,245, shilingi 1,413,904,000 ni michango ya watu binafsi na shilingi 1,556,397,305 ni michango ya wahisani na taasisi mbalimbali za maendeleo . Mwenge wa uhuru mwaka huu unaongozwa na ujumbe usemao “Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na Malaria” Katibu tawala mkoa a...

MWAKALEBELA.................1

Bw. Fredrick Mwakalebela (Kulia) akiwa na Mkewe Bi. Selina Mwakalebela wakati wa mkutano na waandishi wa habari mijini Iringa jana. FREDERICK Mwakalebela mmoja wa wanaCCM anayetafuta ridhaa ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge jimbo la Iringa Mjini amekanusha vikali madai ya rushwa yaliyotolewa dhidi yake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwakalebela alisema hajawahi kukamatwa kwa madai hayo, lakini akakiri kuhojiwa na Takukuru ili atoe ufafanuzi kuhusu taarifa zilizotolewa dhidi yake kwa taasisi hiyo. Akinukuu taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Donasian Kessy kwamba Julai 20 katika kijiji cha Mgongo aliitisha kikao nyumbani kwa Gwido Sanga ambacho kilihudhuriwa na wana CCM 22, Mwakalebela alisema alikutana na wana CCM hao na kutangaza nia yake ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, na kwamba katika kikao hicho hakutoa rushwa ya aina yoyote kama ilivyodaiwa. ...