Skip to main content

Posts

Showing posts from October 5, 2015

MAGUFULI AMSHAWISHI MO KUJENGA KIWANDA SINGIDA ILI KUTOA FURSA YA AJIRA

Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akimwaga sifa kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji baada ya kutumikia vyema na kwa uadilifu kiti chake cha Ubunge jimboni humo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais huyo kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika viwanja wa Peoples mjini humo. Na Nathaniel Limu, Singida MGOMBEA urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli,amemshawishi aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji,kujenga kiwanda mkoani humo, ili pamoja na mambo mengine,kupunguza uhaba wa ajira. Amedai Dewji maarufu kwa jina la MO katika kipindi chake cha ubunge miaka 10 iliyopita, ameonyesha mapenzi makubwa na ya aina yake kwa wakazi wa jimbo la Singida na mkoa kwa ujumla. Dk.Magufuli alisema kutokana na ukweli huo,sasa anapaswa kuhamishia mapenzi hayo kwa kujenga kiwanda mkoani Singida kitakachoajiri vijana, na pia kuinua pato la mkoa na taifa kwa ujumla. Mgombea urais huyo al...

MAGAZETI LEO JUMANNE

KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ATANGAZA KUACHANA NA CCM RASMI

Anasema kamati kuu haiwezi kusema watu watano au sita ni hawa bila kuwasikiliza, kilichotokea mwaka huu ni tofauti kabisa kilichotokea mwaka 1995, safari mwenyekiti ni Jakaya Kikwete, kilichotokea ni jambo kubwa katika historia yetu na mimi katika historia yangu pale ambapo naona kwamba katiba inavunjwa nimekuwa na tabia ya kusema waziwazi na kuwaambia wenzangu si sawa. Mwaka 1972 nikiwa mkuu wa mkoa Simiyu, kulikuwa na Bunge Dar es Salaam, nikakuta kuna mswada wa kurekebisha katika kuhusiana na swala la wakuu wa mikoa. Mchango wangu uliibua hisia kali na kumwambia mwenyekiti muswada aurudishe maana hatuukubali, kwa upande wa watu walipo serikalini walisema ndio na wabunge wa kuchaguliwa walisema hapana. Ilipofika zamu yangu nikasema sina upande, wabunge walifurahi sana. Kura zilipohesabiwa serikali ilishindwa kwa mara ya kwanza katika mfumo wa serikali ya chama kimoja. Mzee Kawawa aliniita akasema wewe ni mwenzetu lakini umetuacha, Rais atakubadilisha kazi. Nil...

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA KUHAMISHA WENGINE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba. Wakuu wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi. Wakuu wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wangingombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kah...