Skip to main content

Posts

Showing posts from February 16, 2017

TUNDU LISSU MAHAKAMA YA KISUTU KESI YA UCHOCHEZI

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salum Hamdani, kueleza anachofahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar , Salum Jecha ana mamlaka ya kufuta matokeo ya uchaguzi au laa. Lissu alihoji hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati Hamdani alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya uchochozi inayomkabili Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio. Mshtakiwa Lissu aliomba kujiwakilisha mwenyewe mahakamani hivyo baada ya ushahidi alimuhoji maswali shahidi kulingana na ushahidi wake. Swali hilo la Lissu lilimfanya Wakili wa Serikali, Paul Kadushi, kupinga akitaka shahidi asijibu kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala Katiba. Kadushi alidai shahidi hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba. Akijibu ping...

NGAYA YA COMORO YAWASILI NCHINI KUMENYANA NA YANGA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1. Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili. Mmoja wa viongozi wa timu hiyo (kushoto), akitoa maelekezo kabla ya kuondoka uwanjani hapo. (Picha na blog ya habari za jamii.com) Wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye gari kuelekea hotelini walikofikia.  Na Dotto Mwaibale KIKOSI cha Timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga katika dimba litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hiyo imewasili leo saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake. Mara baada ya k...

Umoja wa Ulaya watoa Bilioni 22 kusaidia mradi wa Lishe na Usalama wa Chakula

Katika kusaidia Tanzania kuwa moja ya nchi ambazo wananchi wake wana lishe salama, Umoja wa Ulaya (EU) umechangia Euro milioni 9.5 (Tsh. 22 Bilioni) kwa ajili ya kusaidia kutekelezwa kwa mradi wa Lishe na Usalama wa Chakula unaotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wenye thamani ya Euro milioni 24.5 (Tsh. 57.7 bilioni) unaotarajiwa kufanyika katika mikoa ya kanda ya kati. Akizungumza kuhusu msaada huo, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Roeland Van De Geer alisema EU imeamua kusaidia jamii ya Tanzania kupata lishe bora kwani wao wanaamini kuwa pasipo lishe bora mambo mengi ambayo yanahusu maendeleo ya taifa hayawezi kufanyika kwa kasi ambayo yanatakiwa kwenda nayo lakini pia mpango wa kusaidia lishe salama ni moja ya mambo ambayo EU imepanga kusaidia.  Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Roeland Van De Geer akizungumza kuhusu mchango wa Euro milioni 9.5 (Tsh. 22 Bilioni) kwa ajili ya kusaidia kutekelezwa kwa mradi wa Lishe...

African passports: The powerful, the weak and the (now) barred from the US

On Friday US President Donald Trump signed an executive order that barred citizens of seven nations from accessing a US visa to enter the country, effective immediately. Among these are citizens of the African countries Libya, Sudan and Somalia. These countries already have some of Africa’s weakest passports, according to the Arton Capital’s Passport Index, which ranks national passports by how easily they can visit other territories – either without a visa or with a visa on arrival. There are only 37 countries globally a Libyan passport has easy access to, while there are 36 for Sudan and 30 for Somalia (which is ranked the country with the weakest passport in Africa and fifth-weakest in the world). Interestingly these African countries are also some of the world’s least welcoming – meaning they don’t allow many others in visa-free or visa-on-arrival. Somalia is one of only three countries in the world that does not offer any foreign travellers hassle-free entry. Lib...