Skip to main content

Posts

Showing posts from October 25, 2014

Barabara ya Dodoma - Iringa kukuza shughuli za kiuchumi

Gari la kampuni ya ujenzi SIETCO Chengdu, Sichuan-China ikimwagilia maji katika barabara ya Iringa - Dodoma  sehemu ya Iringa mjini ilikupunguza vumbi leo mchana. Barabara ya Iringa-Dodoma yenye urefu wa kilometa 260 unaendelea kukarabatiwa na kujengwa kwa kiwango cha lami kwa ufadhili wa African Development Bank (ADB), Japan Interntional Cooperation (JICA) pamoja na serikali ya Tanzania. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA) Kufunguka kwa barabara kutoka Dodoma hadi Iringa, kutakuza shughuli za kiuchumi na kupunguza umasikini kutokana na barabara hiyo kuwa sehemu ya barabara kuu inayoanzia Cape Town nchini Afrika Kusini kupitia Tanzania hadi Cairo, Misri, maarufu kama The Great North Road. 

CCM JIMBO LA IRINGA MJINI CHA VUNA WANACHAMA WAPYA ZAIDI

Katibu wa CCM Mufindi Miraji Mataturu (kushoto), akimkabidhi mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya mabasi Mlandege leo, zaidi ya wanachama 100 wapya  wajiunga na chama hicho na kukabidhiwa kadi. Katibu wa CCM Mufindi Miraji Mataturu (kulia), akiwaapisha wanachama wapya baada ya kuwakabidhi kadi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya mabasi Mlandege leo, zaidi ya wanachama 100 wapya wajiunga na chama hicho na kukabidhiwa kadi.

WAHITIMU 2228 WA CHUO KIKUU CHA IRINGA WATUNUKIWA VYETI...!

Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na wageni waalikwa muda mfupi baada yakumalizika kwa mahafali ya kwanza ya chuo hicho ambapo jumla ya wanachuo 2228 walitunukiwa vyeti katika fani mbalimbali na mkuu wa chuo hicho Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, akivunja mahafali ya kwanza katika mwaka wa masomo 2013/2014 ambapo jumla ya wanafunzi 2228 wamehitimu. Kulia ni Makamu Mkuu wa Mhuo Prof. Nicholas  Bangu kwenye mahafali hayo. chuo kikuu cha iringa   Mkuu wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma na waziri mstaafu wa Elimu Joseph Mungai wakifuatilia mahafali leo. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (Master in Business Administration in Entrepreneurship and Marketing) Patrock Tenywa ambaye pia ...

Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda wakamilika

Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda,  Mkoa wa Katavi Seneti Lyatuu akiwaonesha timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda. Nyuma yake (mwenye suti nyeusi) ni Mhandisi Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge Tanzania, Makao Makuu, Dar es Salaam. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda  Bw.  Seneti Lyatuu akifafanua jambo wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanja hicho. Barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi. Na Mwandishi wetu, Mpanda Serikali imekamilisha ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwa...

SERIKALI YAWEKA TARATIBU ZA KUZINGATIA ILI KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA WAMILIKI HALALI WA LAINI ZA SIMU

Meneja mawasiliano wa  TCRA,    Innocent Mungy  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO Mwanadamu ameumbwa na kuzaliwa akiwa na asili ya kuwa na uwezo na upeo unaomuwezesha kuwasiliana baina ya mtu na mtu kunzia ngazi ya familia, jamii inayomzunguka, taifa na hatimaye ulimwengu mzima. Akiwa na mamlaka ya kutumia mawasiliano katika maisha yake ya kila siku, mwanadamu anayatumia mawasiliano hayo kama mchakato wa kuhamisha na kupashana taarifa ama habari kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa nyakati tofauti tofauti.

Uboreshaji wa Daftari kuanza

Makamu Mwenyekiti wa    Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), pia  na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Hamid      Mahamoud Hamid (kushoto)   akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba. Baadhi    ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na waandishi    wa habari kuhusu    taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julias Malaba. icha zote na Magreth Kinabo- Maelezo.

Acting Republican President Lungu leads in celebrating golden jubilee

ACTING Republican President Edgar Lungu yesterday led hundreds of patriotic Zambians and former Republican Presidents at the freedom statue in laying wreaths in remembrance of all fallen heroes. Mr. Lungu who first layed the wreath at the Statue later saw First republican president Dr. Kenneth Kaunda to lay his wreath followed by his fourth republican counterpart, Rupiah Banda.

MAGAZETI LEO JUMAMOSI