Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela askari polisi, Sajenti Rogers Mmari, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuua bila kukusudia katika tukio lililosababisha kifo cha Nashon Kiyeyeu (23). Hukumu hiyo ilitolewa Machi 19, 2026 na Jaji Angaza Mwipopo, kufuatia mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka uliothibitisha kuwa mshtakiwa alihusika na kifo cha Kiyeyeu, mkazi wa Nyamhanga, Manispaa ya Iringa. Katika kesi hiyo, ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 14, 2024 katika eneo la Ipogoro, ambapo marehemu alishambuliwa na askari huyo kwa kushirikiana na mgambo, Thomas Mkembela, hali iliyosababisha kupoteza maisha yake. Tukio hilo lilihusishwa na tuhuma za wizi wa simu ya mkononi inayodaiwa kuwa ya Beatrice Baraka Kimata. Akisoma hukumu, Jaji Mwipopo alisema ushahidi uliowasilishwa haukuonesha kuwepo kwa nia ya moja kwa moja ya kuua, hivyo mahakama ikamtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia chini ya vifungu namba...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.