Skip to main content

Posts

Showing posts from March 21, 2026

Ugonjwa wa Mapele Ngozi kwa Ng’ombe Kupatiwa Ufumbuzi

Daktari wa Mifugo Mfawidhi wa ZVC Iringa, Dkt. Jeremia Choga (L) wakati wa zoezi la uchukuaji sampuli.  Na Friday Simbaya, Iringa   Ugonjwa wa Mapele Ngozi (Lumpy Skin Disease - LSD) umeendelea kuwa miongoni mwa magonjwa hatari yanayoathiri mifugo, hususan ng’ombe, na kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji kutokana na gharama za matibabu na vifo vya wanyama.   Hivi karibuni, ugonjwa huo umeripotiwa kushambulia maeneo ya Nyanda za Juu Kusini, hasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe, hali iliyosababisha taharuki kwa wafugaji. Takwimu zinaonesha kuwa takribani ng’ombe 750 wameathirika na baadhi kufa katika kipindi cha Februari hadi Machi, 2026 wilayani humo.   Kufuatia mlipuko huo, Serikali kupitia wataalamu kutoka Kituo cha Huduma za Mifugo Nyanda za Juu Kusini (ZVC Iringa) na Taasisi ya Chanjo za Mifugo Tanzania (TVI), wameweka kambi wilayani Momba kwa ajili ya kufuatilia hali ya ugonjwa huo na kuchukua sampuli kutoka kwa wanyama walioathirika.   ...