Skip to main content

Posts

Showing posts from March 3, 2026

Wanawake Wahimizwa Kujitokeza Samia Ardhi Kliniki Iringa

Iringa. Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Machi 8, wananchi mkoani Iringa, hususan wanawake, wamehimizwa kujitokeza kwa wingi katika huduma za ‘Samia Ardhi Kliniki’ ili kunufaika na huduma mbalimbali za masuala ya ardhi. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kasper Mmuya, anatarajiwa kuzindua rasmi kliniki hiyo Machi 4, 2026 katika Viwanja vya Garden Posta, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Rai hiyo imetolewa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Iringa, Bi. Rehema Kilonzi, katika mahojiano maalumu ofisini kwake. Amesema kliniki hiyo inalenga kutoa elimu, ushauri na huduma za haraka kwa wananchi kuhusu masuala ya umiliki na usimamizi wa ardhi. “Wananchi wafike kwa wingi katika viwanja vya Garden Posta ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa, ikiwemo elimu na ushauri wa masuala ya ardhi, utoaji wa hatimiliki papo kwa papo, makadirio ya kodi ya pango la ardhi pamoja na uhuishaji wa miliki zilizoisha muda wake,” alisema Kilo...