Skip to main content

Posts

Showing posts from October 5, 2016

SERIKALI YARUHUSU WIMBO WA CHURA WA MSANII SNURA KUPIGWA

Snura Mushi Msemaji wa Msanii Snura Baraka Nyagenda akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo. Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda. Mkutano na wanahabari ukiendelea. N a Dotto Mwaibale SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura wa msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi alisema wimbo wake na video umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura kufanyiwa marekebisho na kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania. Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa barua iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye kumbukumbu HA.26/37...

FAST JET YAANZISHA SAFARI ZA NDEGE MPYA NCHINI

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 kusafirisha abiria. Kulia ni Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro. Ofisa Uhusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Lucy Mbogoro (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse (katikati), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Christina Kausan. Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Dotto Mwaibale WANANCHI wametakiwa kuchangamkia usafiri wa ndege wa Kampuni ya Fast jet baada ya kampuni hiyo kuanza kutumia ndege mpya aina ya Embraer 190 ambayo ni nafuu zaidi kwa matumizi. Mwito huo umetolewa na Dar es Salaam leo na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Fast jet, John Corse wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuwa ndege hizo ni rahi...