Mbarali. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jamhuri iliyopo Kijiji cha Ilongo, Kata ya Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wameanza kunufaika na mradi wa maji safi uliotekelezwa na Rufiji Basin Water Board kupitia Mradi wa NBS-USANGU. Kabla ya utekelezaji wa mradi huo, wanafunzi walilazimika kutembea zaidi ya kilometa tatu kutafuta maji, hali iliyokuwa ikiathiri mahudhurio yao, kuongeza uchovu na kuchelewesha masomo. Wengine walilazimika kufika shuleni wakiwa wamechoka, jambo lililopunguza umakini darasani. Kupitia mradi huo, kisima kirefu kimechimbwa na maji kusambazwa moja kwa moja shuleni pamoja na kwa wananchi wa maeneo jirani, hatua iliyoboresha mazingira ya kujifunzia na kuimarisha usalama wa wanafunzi. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi hivi karibuni , Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Jenifer Sanga, alisema upatikanaji wa maji ndani ya shule ni mabadiliko makubwa kwa ustawi wa wanafunzi. “Hii ni faraja kubwa kwetu. Sasa wanafunzi hawatapoteza muda kutafuta maji na watawe...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.