Skip to main content

Posts

Showing posts from April 27, 2014

MAGAZETI LEO JUMATATU

KWA HISANI YAMJENGWABLOG.COM 

Ukawa wapata pigo

' Bunge Maalumu la Katiba, jana liliridhia azimio la kuzifanyia marekebisho kanuni zake saba bila kuwapo kwa wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wamesusia Bunge hilo.

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YAFANA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC. (PICHA:FREDDY MARO) Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru kuwaongoza watanzania katika maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka Aprili 26 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili mwaka 1964 watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo wakiwemo viongozi mbalimbali na marais wa nchi mbalimbali za Afrika na wawakilishi wa nchi mbalimbali pia katika mataifa mbalimbali ya Ulaya,   Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Yoweri Mseveni wa Uganda katikati nI King Mswati wa Swaziland na kushoto ni Rais Pie...

‘Ushirikina’ Wakwamisha Mapambano ya Mimba kwa Wanafunzi Mbeya Vijijini

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini. Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati) akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake. Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi. VITISHO na hofu ya vitendo vya ushirikina imebainika kuwa vikwanzo vya mapambano ya baadhi ya watu wanaowatia mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya.

(CCM) kimepanga mkakati wa kuengua wataka urais wanaume

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga mkakati mpya wa kuengua wataka urais wanaume kwa kuingiza hisia za kijinsia kama walivyofanya kumdhibiti aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta, alipotaka kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2010. Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa mkakati huo unalenga zaidi kumng'oa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye anaonekana tishio kwa wenzake wanaotajwa kutaka urais. Kwa mkakati huo, kundi la wana CCM walio karibu na Rais Jakaya Kikwete, wameanza kuzungumzia jinsi ya kumpitisha Dk. Asha-Rose Migiro agombee urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

WAZIRI WA ARDHI PROF.TIBAIJUKA AKUTANA NA WAZIRI MAMBO YA NJE YA USHELISHELI FAURE

Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo.Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania. Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) akizungumza na Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka (Kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Pembeni yao ni Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje. Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka akizungumza (Kushoto) wakati Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) wakati alipotembelea Wizara hiyo jij...

Magazeti Leo Jumapili