Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2016

WANANCHI KILOLO WATAKA SERIKALI IWAPATIE CHETI CHA ARDHI YA KIJIJI

KILOLO: WANANCHI wa kijiji cha Mawala, kata ya Irole katika Wilaya ya Kilolo  mkoani Iringa wameitaka serikali wilayani humo kuharakisha upimaji wa  maeneo ya ardhi ya kijiji chao pamoja kupatiwa cheti cha ardhi ya  kijiji ili kupunguza migororo mbalimbali iliyopo kwa sasa. Wakizungumuza jana katika mdahalo walisema serikali kwa kutumia sheria  ya ardhi ya vijiji itenge maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji  hatua itakayosaidia makundi hayo kuepukana na migogoro kwa kuwa  makundi yote mawili yanategemeana. Mdahalo huo uliozungumzia namna ya kuondoa migogoro ya ardhi ya kijiji  uliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Grassroots Oriented Development (TAGRODE) yenye makao yake makuu mjini Iringa kwa  shirikiana na PELUM Tanzania . Wakichangia mada, wakazi hao wa Kijiji cha Mawala walisema migogoro ya  ardhi katika maeneo yao itakoma kama serikali itasimamia kwa nguvu  zake zote utekelezaji...

WAZIRI NCHEMBA AZUKA IDARA YA NIDA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Mwigulu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (watano kushoto) akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika hotuba yake fupi kwa Waziri Mwigulu, alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi D...

HATIMAYE MPEMBA WA MAGUFULI ABURUZWA MAHAKAMANI,NI YULE JANGILI WA MENO YA TEMBO

Hatimaye Vinara wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa kukusanya, kuuza vipande 50 vya meno ya tembo, vyenye thamani ya Sh. milioni 392.8 wamepandishwa katika mahakamani wakikabiliwa na mashtaka manne ya kuhujumu uchumi akiwamo, Yusuf Ali maarufu kama Shehe ama "Mpemba" (35). Mbali na "Mpemba", washtakiwa wengine n mfanyabiashara mkazi wa Mrimba, Mkoani Morogoro, Charles Mrutu maarufu Mangi Mapikipiki ama Mangi Mpare (37), wakazi wa Dar es Salaam, Benedict Kungwa (40) Jumanne Chima maarufu Jizzo ama JK (30), Pius Kulagwa (46) na Dereva wa Vikindu, Pwani Ahmed Nyagongo (33). Washtakiwa wote walisomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.Wakili wa Serikali Paul Kadushi, alidai kuwa kati ya Januari, mwaka 2014 na Oktoba, mwaka huu maeneo tofauti Mkoani Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Tanga na Mtwara washtakiwa wakiwa na wenzao ambao bado hawajashtakiwa mahakamani, walijihusisha...

POMBE FEKI ZA VIROBA ZALITESA TAIFA,WAZIRI WA MAGUFULI AKIFUMA KIWANDA BUBU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kukama shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo hayo. Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar es Salaam.  Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa. Kwa hatua hiyo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee n...

LOWASSA ATOA SABABU YA KUTOKUWEPO KWENYE MSIBA WA SITTA NA MUNGAI

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoonekana kwenye misiba ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri wa Elimu wa zamani, Joseph Mungai. Sitta alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani alipokuwa ameenda kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata alifariki Mungai. Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria kwakuwa alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake, Bahati Lowassa. “Mdogo wangu Bahati Lowassa ni ofisa ubalozi nchini Afrika Kusini, alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa. Kwa siku zote nilikuwa huko kumuangalia. Nisingeacha kuhudhuria misiba hiyo,”Lowassa  Mwanasiasa huyo ameongeza kuwa alikuwa pamoja na waombolezaji kwa kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sitta kupitia vyombo vya habari pamoja na kumtumia mwanasheria wake kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa familia ya Mungai.