Skip to main content

POMBE YA WANZUKI YA BORESHA MAISHA YA KINAMAMA


KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanzisha mradi wa kupika pombe aina ya Wanzuki kwa ajili ya kuwezeshana wenyewe kwa wenyewe. Kikundi hiki cha Upendo kipo katika Mtaa wa Lipinyapinya, Peramiho ‘B’ Wilaya Songea mkoani Ruvuma.
Kinywaji baridi cha wanzuki hutengenzwa kwa kutumia maji, majani ya chai, sukari na amila na kusindikwa kwenye chupa mbalimbali zikiwemo za soda, bia na maji.
Mweyekiti wa Kikundi  cha Upendo Bi. Asumpta  Luoga alisema kuwa kikundi hiki kilianza tarehe  5 May, 2011 kikiwa na wanachama wachache  kwa mboga  za majani hasa Chinese, na kwa sasa kina jumla ya wanachama 20.
“Tulianza kwa kuuza Chinese baada ya kuona kuwa mtaji umekuwa kidogo tukaachana na biashara hiyo na kubuni biashara nyingine japo tulianza kutengeneza pombe ya kiyenyeji aina ya Wanzuki” alisema Bi. Luoga.


Pombe hii ya Wanzuki malighafi yake ni pamoja na maji, sukari, majani ya chai na amila kwa kupika  mchanganiko huo kwenye moto na baada yapo kusindikwa kwenye chapa mbalimbali zikiwemo za soda, bia na makopo ya maji.
Ingawa kiwango cha alcohol bado hakijafahamika sawa sawa, pombe hii  kali kipimo chake ni  kikombe cha robo lita na kinauzwa kwa bei ya Shilingi 200/- kwa chupa.
Aidha, mwenyekiti huyo alisema kuwa kikundi chao kinaundwa na makundi matatu muhimu kama vile waathirika wa Ukimwi, Wajane na Yatima.  Alisema kuwa kinywaji baridi aina ya Wanzuki hupikwa kwa pamoja na baada ya mauzo kupatikana mwanachama wanamtoa kwa kumpa katika Shilingi 25,000/- hadi Shilingi 30,000/- kila baada ya siku nne. Mzinguko huu wakipeana pesa unaendelea hadi kila moja anapata mgao wake.
“Huwa tunamtoa mwanachama mmoja kwa kumpa kiasi cha 25,000/- hadi 30,000/- kutegemea na biashara ili aweze kununua vyombo vya nyumbani na mauzo yakiwa zaidi  huwa tunaweka kwenye akiba ili kutunisha mfuko.  Kwa kweli kamradi ketu haka huwa  kanatusaidia kidogo kidogo kuliko kukaa tu ukilinganisha maisha kuwa magumu bila kufanya biashara hautaweza  kuishi,” alisema Bi. Luoga.
Kwa upande wa Katibu wa Kikundi hicho Bi. Anitha Komba alisema kuwa pamoja na kuwepo baadhi ya mafanikio pia kuna changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kama  kikundi ikiwa ni pamoja na upungufu wa vifaa kama vile madumu ya maji, chupa, viti vya kukalia wateja, meza, radio, majiko ya kisasa na mabanda.
Alisema kikundi kinahitaji vitu kama hivyo ili viweze  kuwasaidia katika shughuli zao,  kama vile majiko ya kisasa yaliyokuwa rafiki wa mazingira ili wapunguze matumizi ya kuni, wanahitaji mabanda kwa ajili ya kuuzia biashara hiyo na radio kwa muziki na burudani kwa wateja n.k.
“Hatuna sehemu maalum ya kuuzia biashara yetu kwa hiyo tunalazimika kupeleka kwenye vilabu vya pombe vya watu wengine lakini nasi tungekuwa na sehemu yetu maalum tunaweza kufanya biashara yetu kwa uhuru kuliko hivi sasa tunahangaika sehemu ya kuuzia,” alisema Katibu wa kikundi.
Aidha, Katibu huyo aliwataja wanachama kuwa ni pamoja na Agata Mbano, Brandina Mbawala, Fausta Haule, Amina Pili, Maria Ngonyani, Jisela Chale, Salome Nyoni na Osmundi Kayombo.
Wengine ni Rose Nyoni, Agnes Ndauka, Aifosia Mbano, Evans Mbano, Romana Mbilo, Mage Kayombo, Avena Mahundi, Charles Ponela na Sebestian Nyoni.
Naye Mweka Hazina wa Kikundi cha Upendo, Bi. Joyce Kunguru alisema kuwa mpaka sasa kikundi kina akiba ya shilingi 25,000/- tu, na  wanaomba wafadhili mbalimbali wajitokeze ili waweze kuwasaidia ili waweze kupanua biashara yao pamoja na kuongeza wanachama.
“Tunaomba wafadhili waweze kusikia kilio chetu kwa kutusaidia katika kutuwezesha ili tuweze kuongeza mtaji wetu na hatimaye tuweze kuongeza wanachama wengi zaidi. Kama unavyojua mwanamke ni nguzo kuu katika familia na mzalishaji mkuu pia, kwa hiyo akiwezeshwa anaweza  kupunguza umaskini wa kipato,” alisema Bi. Kunguru.
 Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...