Skip to main content

DC LUDEWA AITAKA HALMASHAURI KUTUNGA SHERIA NDOGONDOGO ZA MADINI ILI KUJIONGEZEA MAPATO


Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa Bi. Georgina Bundala ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kutunga sheria ndogondogo (by laws) ili kujipatia mapato kupitia watafiti na wachimba madini wanaoingia wilayani humo kila kukicha.
Bi Georgina aliyasema hayo jana  ofisini kwake alipotembelewa na mwandishi aliyotaka kujua ni nini mchango wa watafiti na wachimba madini waliopo katika maeneo mbalimbali wilayani mwake kwa wilaya yake.
Bundala alisema anashangaa kuona Baraza la Madiwani chini ya wabunge wawili wasomi na wanasheria kunyamaza kimya bila kuibua mjadala kuhusu kutunga sheria ndogondogo zitakazoingizia halmashauri yao kipato.
“Halmashuri ya Wilaya ya Ludewa inaweza kujiongezea kipato kupitia watafiti na wachimbaji madini waliopo katika maeneo mbalimbali kwa kutunga sheria ndogondogo zitakazo wabana wadau hao,” alisema mkuu huyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Kongo alipotakiwa na Nipashe kujibu kwanini Baraza lake limekaa kimya katika suala zima la kutunga sheria ndogondogo zikiwemo za kuingiza mapato kupitia watafiti na wachimba madini alisema mchakato huo ulishafanyika na kuwasilishwa kwa waziri mwenye dhamana.
Bw. Kongo alisema siyo sheria za madini tu zilizopelekwa kwa waziri kwa ajili ya kusainiwa bali zipo na zingine zinazohusu masuala mengine muhimu labda mkuu wa wilaya hajawahi kuziona.
Alto Liholelu ni mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa akizungumza kwa njia ya simu akiwa Dar es salaam, alisema  tayari waziri ameshasaini na kinachosubiriwa kuchapishwa kwenye gazeti la serikali ili zianze kutumika.
“Mbali na makampuni ya madini kulipa ada na ushuru mwingine kila mwaka makampuni hayo yatatakiwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama vile maji, elimu na afya,”alisema mwanasheria huyo.
Bw. Liholelu alisema mchakato huo ulifanyika mwaka jana na kwamba sheria zilizokwishatungwa na kupitishwa na Baraza la madiwani ni pamoja na sheria ya ada na ushuru na mfuko wa elimu.
Alizitaja sheria zingine zinazotaraji kupitishwa na halmashauri kuwa ni pamoja na sheria ya kilimo na kwamba sheria hii itadhibiti masoko ya mazao ya kilimo kwa kila kijiji kuwa na kituo kimoja cha kuuzia na kununua badala ya walanguzi kufuata mazao shambani.


Comments

Popular posts from this blog

Four Armed Robbery Suspects Killed In Shootout With Police In Songwe

  “This is Vwawa Bus Stand, where the incident occurred in which armed robbers shot and killed a security guard before fleeing with various items.” Songwe. Four suspected armed robbers have been shot dead following a confrontation with police in Songwe Region after allegedly being involved in a violent raid on a mobile phone and financial services shop in Vwawa town, Mbozi District, in which a security guard was killed. According to a statement issued today, December 30, 2025, by the Songwe Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police (SACP) Augustino Senga, the incident occurred at around 3:30 a.m. The suspects reportedly stormed the shop, owned by businessman Gabriel Msemwa, at the Vwawa main bus stand, killed the guard, William Mwampashi (45), and fled with assorted items. The deceased suspects have been identified as Bruce Mwasenga, Eliuta Mapunda, Abdul Chiba, and Justine, known by a single name. SACP Senga said police immediately launched intensive, inte...

JAB Yawasogeza Huduma Waandishi Iringa, Yaomba Ushirikiano Kudhibiti Waandishi Wasioidhinishwa

Iringa. Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeendelea na jitihada za kusogeza huduma zake kwa waandishi wa habari nchini, safari hii ikifika katika Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (Iringa Press Club – IPC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha tasnia ya habari na kulinda taaluma ya uandishi wa habari. Akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari mkoani Iringa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusu majukumu ya bodi, mchakato wa ithibati pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili waandishi wa habari ngazi ya mikoa. Wakili Kipangula amesema bado kuna changamoto ya uwepo wa watu wanaojihusisha na shughuli za uandishi wa habari bila kuwa na ithibati halali, hali inayochafua tasnia na kuhatarisha maadili ya kazi hiyo nyeti. “Tunawaomba waandishi wa habari kushirikiana na Bodi kwa kuwafichua watu wanaojitambulisha kama waandishi bila kuwa na ithiba...

MUCE IMPLEMENTS SH18.6 BILLION PROJECT IN HONOUR OF FATHER OF THE NATION’S VISION

Iringa. As Tanzania marks 26 years since the passing of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere — a passionate advocate for education — Mkwawa University College of Education (MUCE), a constituent college of the University of Dar es Salaam (UDSM), continues to successfully implement the Higher Education for Economic Transformation (HEET) Project worth over Sh18.6 billion. Speaking to journalists in Iringa, MUCE Principal Prof Method Samwel Semiono said the project, implemented by the government through the Ministry of Education, Science and Technology, aims to reform the higher education system so it can directly contribute to the country’s economic transformation. “The five-year project (2021/2022–2025/2026) is funded by the World Bank and focuses on curriculum improvement, infrastructure development, human resource capacity building, inclusive education and gender equality, as well as promoting the use of ICT and digital learning,” explained Prof Semiono. He no...